Rais wa Tunisia awafukuza kazi darzeni ya majaji

Rais wa Tunisia Kais Saied

Rais wa Tunisia Kais Saeid amewafuta kazi majaji 57 akiwashutumu kwa  rushwa na kuwalinda magaidi.

Katika hotuba yake kwenye televisheni amesema alitoa fursa kadhaa na maonyo kwa mahakama kujirekebisha.

Miongoni mwa waliofutwa kazi na kutangazwa katika gazeti la serikali Gazette ni Youssef Bouzaker mkuu wa zamani wa baraza la mahakama ya juu.

Rais Saied alibadilisha baraza hilo mwaka huu ikiwa ni sehemu ya juhudi zake kuimarisha nafasi yake baada ya kuingia madarakani mwezi Julai mwaka 2021.

Tayari amefuta bunge la Tunisis na kuweka pembeni katiba. Ameahidi kufanyika kura ya maoni kwa ajili ya katiba mpya mwezi ujao.

Vyama vya upinzani na jumuiya ya biashara wanapinga hatua hiyo.