Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 20, 2024 Local time: 06:25

Chama cha wafanyakazi chakataa kushiriki mjadala wa kitaifa, Tunisia


Waandamanaji wa Tunisia kwenye picha ya awali
Waandamanaji wa Tunisia kwenye picha ya awali

Chama kikubwa cha wafanyakazi nchini Tunisia, cha UGTT kimesema Jumatatu kwamba hakitoshiriki kwenye mjadala wa kitaifa ulioitishwa na rais Kais Saied, kwa madai kwamba masuala mengi muhimu ya kijamii hayajazingatiwa.

Saied alivunja seriali yake Julai mwaka jana kabla ya kuvunja bunge pia na kujitwalia madaraka yote, hatua iliozua ukosoaji mkubwa kutoka kwa wapinzani wake, wakisema kwamba ni mapinduzi dhidi ya nchi pekee iliokuwa na demokrasia baada ya mapinduzi ya kiarabu.

Kwa mujibu wa shirika la habari la AP. Kiongozi huyo amekuwa akikwepa kufanya mashauriano na vyama vya kisiasa wakati kukiwa na shinikizo la kimataifa kwamba ahusishe washika dau wote. Ijumaa iliyopita Saied aliteua profesa mmoja wa sheria mtiifu kwake ili kuongoza jopo maalum lililotwikwa jukumu la kuandika upya katiba kupitia mjadala wa kitaifa.

Chama cha wafanyakazi cha UGTT kilikuwa miongoni ya makundi yaliochaguliwa kushiriki wakati vyama vya kisiasa vikitengwa. Hata hivyo chama hicho chenye zaidi ya wanachama milioni moja kimekataa mwaliko huo, hatua inayoonekana kuwa changamoto kubwa kwa Saied.

XS
SM
MD
LG