Kulingana na taarifa rasmi ya serikali, kutakuwa na swali moja, watakaloulizwa wapiga kura iwapo wanakubali katiba mpya.
Taarifa hiyo imesema kwamba vituo vya kupigiwa kura vitafunguliwa saa kumi na mbili asubuhi na kufunga saa nne usiku.
Tangazo hilo limekuja baada ya rais Kais Saied kuitaja kamati ya ushauri kusimamia utekelezaji wa katiba mpya licha ya pingamizi za kutaka hatu ahiyo kubatilishwa.
Vyama vikuu vya upinzani vivmesema kwamba vitasusia majadiliano ya kupitishwa kwa katiba mpya.
Kais Saied ametekeleza mabadiliko makubwa yanayolenga kumpa madaraka zaidi, ikiwemo kufuta taasisi kadhaa na kulivunja bunge.
Facebook Forum