Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 02, 2024 Local time: 07:26

Wachache wajitokeza Tunisia katika maoni ya katiba


Rais wa Tunisia katika mkutano wa Umoja wa Ulaya na Umoja wa Afrika huko Brussels Ubelgiji.
Rais wa Tunisia katika mkutano wa Umoja wa Ulaya na Umoja wa Afrika huko Brussels Ubelgiji.

Wakati rais wa Tunisia anajiandaa kuandika upya katiba baada ya kulifuta bunge mwaka jana na kuongoza kwa kutumia amri, amewataka  wananchi kutoa maoni yao kwa kuandaa  maswali ya hiari ya kuchagua  kwa njia ya mtandao.

Huku zikiwa zimesalia wiki mbili kabla ya kukamilika kwa maswali hayo kujibiwa , ni watu 276,000 pekee ambao wameshiriki katika nchi hiyo yenye watu milioni 12, kulingana na tovuti ya utafiti huo, huku kukiwa na shutuma za wakosoaji wa Rais Kais Saied kwamba mashauriano hayo ni kama utani.

Baada ya hatua yake ya kupinga bunge lililochaguliwa majira ya kiangazi mwaka jana, kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 64 alitangaza mwezi Desemba kuwa atateua kamati ya kuandika upya katiba hiyo pamoja na maoni ya wananchi na kuipigia kura ya maoni mwezi Juni.

Anasema uingiliaji kati wake ulikuwa jibu kwa muongo mmoja wa kudorora kisiasa na kiuchumi mikononi mwa wasomi mafisadi na wanaojitumikia wenyewe.

XS
SM
MD
LG