Alitoa taarifa hiyo kwenye mkutano na baraza la usalama wa kitaifa, saa chache baada ya wabunge kufanya kikao kwa njia ya mtandao na kupitisha mswada wa sheria unaopinga hatua za dharura zilizochukuliwa na rais Saied mwaka jana.
“Leo, katika wakati huu wa kihistoria, natangaza kuvunja bunge la wawakilishi wa wanainchi, ili kuilinda nchi na taasisi zake,” alisema katika taarifa yake iliyopeperushwa kwenye televisheni ya taifa.
Amelaani hatua ya bunge na kuitaja kuwa jaribio la mapinduzi, na kusema kwamba wahusika walilisaliti taifa.
Amesema “ Watafunguliwa mashtaka ya uhalifu.”
Muhadhiri huyo wa zamani wa masomo ya sheria, ambaye alichaguliwa mwaka wa 2019 kufuatia hasira ya wanainchi dhidi ya wanasiasa, tarehe 25 Julai mwaka jana, aliifuta serikali, kusimamisha bunge na kujipatia mamlaka mbali mbali.
Facebook Forum