DRC : Fayulu awataka wafuasi wake kuandamana kupinga matokeo

Martin Fayulu

Mgombea wa upinzani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) Martin Fayulu, Jumapili, amewataka wafuasi wake kuandaa maandamano kupinga matokeo ya uchaguzi wa urais baada ya Mahakama ya Katiba kukataa shauri lake la kukataa matokeo hayo.

Mgombea wa upinzani Felix Tshisekedi tayari Jumamosi alitangazwa kuwa mshindi wa uchaguzi wa Disemba 30, 2018.

Vyanzo vya habari nchini DRC vinaendelea kuripoti kuwa Fayulu anaendelea kudai kuwa Tshisekedi alifanya makubaliano ya kuunda serikali ya pamoja na rais anaye ondoka madarakano Joseph Kabila.

Lakini timu ya uchaguzi ya Tshisekedi inakanusha hilo.

Wafuasi wa Tshisekedi walijitokeza katika mitaa ya Kinshasa baada ya uamuzi wa Mahakama mapema majira ya asubuhi Jumapili kusheherekea ushindi wao.