Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Mei 02, 2024 Local time: 07:05

Zelenskyy asema maelfu ya wakazi wa kusini mwa Ukraine hawana maji ya kunywa baada ya bwawa kulipuliwa

Mafuriko yaliyotokea katika eneo la Kherson baada ya bwawa la Kakhovka kulipuliwa.
Mafuriko yaliyotokea katika eneo la Kherson baada ya bwawa la Kakhovka kulipuliwa.

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy amesema Jumatano maelfu ya watu hawana maji ya kunywa, siku moja baada ya kulipuliwa kwa bwawa la Kakhovka kusini mwa Ukraine.

Zelenskyy aliandika kwenye ukurasa wake wa Twitter kwamba uharibifu wa bwawa hilo ulikuwa wa makusudi kabisa huku akiwalaumu wanajeshi wa Russia.

Rais pia ameishutumu Moscow zaidi kwa kutochukua hatua kusaidia wale wanaoishi katika maeneo yaliyo chini ya udhibiti wao ambao sasa wanakabiliana na athari za mafuriko.

Waokoaji wakiwaondoa watu katika eneo la mafuriko baada ya bwawa la Nova Kakhovka kulipuliwa, huko Kherson, Ukraine, Juni 7, 2023.
Waokoaji wakiwaondoa watu katika eneo la mafuriko baada ya bwawa la Nova Kakhovka kulipuliwa, huko Kherson, Ukraine, Juni 7, 2023.

Maafisa wa Ukraine walisema zaidi ya watu 17,000 walikuwa wakihamishwa kutoka maeneo kando ya Mto Dnipro.

Wakati huo huo takriban miji na vijiji 40 vilikuwa vimefurika maji katika maeneo yaliyo chini ya udhibiti wa Ukraine kufuatia shambulizi hilo.

Mitaa ya Kherson, Ukraine yafurika maji Juni 7, 2023 baada ya kuta za bwawa hilo kubomoka.
Mitaa ya Kherson, Ukraine yafurika maji Juni 7, 2023 baada ya kuta za bwawa hilo kubomoka.

Zaidi ya watu 900 walihamishwa kutoka maeneo yanayokaliwa na Russia.

Forum

XS
SM
MD
LG