Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Mei 02, 2024 Local time: 10:38

UKRAINE: Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani asema njia pekee ya kusitisha mapigano ni kupatikana amani ya 'haki na ya kudumu'


Antony Blinken
Antony Blinken

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken anasema hakuna njia ya inayowezekana kusitisha mapigano katika vita nchini Ukraine mpaka iwe ni sehemu ya kile alichokiita makubaliano ya amani yaliyo na“haki na ya kudumu” ikiwemo majeshi ya Russia kuondoka Ukraine.

Akiongea huko Helsinki, Finland, mwanachama mpya wa umoja wa NATO, Blinken alisema “kusitisha vita kwa kuacha hali ibakie kama ilivyo hivi sasa katika mstari wa mbele” itamruhusu Rais wa Russia Vladimir Putin kuendelea kujiimarisha kudhibiti eneo hilo ambalo amelikamata siyo “amani ya haki na ya kudumu” na inawapa Moscow na “wengine wanaotaka kufanya ubabe duniani” ujumbe potofu.

Blinken aliongeza kuwa Marekani itaendelea kushawishi juhudi za amani zinazofanywa na nchi nyingine ilimradi wanasimama kutekeleza mkataba wa Umoja wa Mataifa na kuheshimu haki ya Ukraine kujitawala, mipaka yake na uhuru wake.

Wakati huo huo, maafisa nchini Ukraine Ijumaa walisema jeshi la nchi hiyo limetungua makombora 30 na ndege zisizo kuwa na rubani za Russia katika anga ya Kyiv.

Taarifa ya jeshi la anga ilisema mifumo ya ulinzi wa anga ilitungua makombora ya masafa marefu na ndege 21 zisizokuwa na rubani.

Maafisa walisema watu wasiopungua wawili walijeruhiwa kutokana na mabaki ya makombora na ndege hizo zilizotunguliwa.

Forum

XS
SM
MD
LG