Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Oktoba 02, 2023 Local time: 22:17

Mapigano yanaendelea Ukraine katika maeneo ya Zaporizhzhia; asema Kuleba


Waziri wa Mambo ya Nje wa Ukraine, Dmytro Kuleba

Waziri wa mambo ya nje wa Ukraine, Dmytro Kuleba alielezea kua na imani kwamba mashambulizi yaliyopangwa na Ukraine dhidi ya Russia yatageuza wimbi la vita na itairuhusu Ukraine kurejesha ardhi zake kutoka Russia

Mapigano yanaendelea katika maeneo kadhaa ya mstari wa mbele wa mapigano nchini Ukraine katika mkoa wa Zaporizhzhia na Donetsk siku ya Jumatatu ikiashiria kuanza kwa mashambulizi ya Ukraine yaliyokua yanatarajiwa kwa muda mrefu.

Wakati wa mahojiano mjini Kyiv, Waziri wa Mambo ya Nje wa Ukraine, Dmytro Kuleba alisema Ukraine iko tayari na silaha zilizokua zikitarajiwa kwa muda mrefu kuanza mashambulizi yake dhidi ya Russia lakini bado imekaa kimya kuhusu kama mashambuliyo tayari yameanza au lini yataanza.

Kuleba alielezea kua na imani kwamba mashambulizi yaliyopangwa na Ukraine dhidi ya Russia yatageuza wimbi la vita na itairuhusu Ukraine kurejesha ardhi zake kutoka Russia. Alisema ushindi kama huo utafungua njia kwa Ukraine kujiunga na NATO. Uanachama katika muungano wa kijeshi, labda utawezekana tu kwa Ukraine baada ya kumalizika kwa uhasama, alisema.

Wanajeshi wa Ukraine wamekuwa wakiongeza operesheni za mashambulizi dhidi ya Russia katika mpaka wa mikoa ya Zaporizhzhia na Donetsk nchini Ukraine. Lakini Kyiv ilipuuzilia mbali ripoti za Russia kwamba mashambulizi hayo yameanza na kwamba jeshi la Russia lilizuia mashambulizi makubwa ya Ukraine katika mkoa wa Donetsk.

Forum

XS
SM
MD
LG