Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Mei 05, 2024 Local time: 00:28

Russia inasema wanajeshi wake 71 waliuawa katika mashambulizi ya Ukraine


Waziri wa ulinzi wa Russia Sergei Shoigu
Waziri wa ulinzi wa Russia Sergei Shoigu

Jeshi la Russia Jumanne limekiri kuwa wanajeshi wake 71 waliuawa katika operesheni za kujibu mashambulizi ya Ukraine kwenye uwanja wa mapambano siku tatu zilizopita, ikiwa jambo la nadra kwa Moscow Kutoa taarifa za wanajeshi wake waliouawa.

Waziri wa ulinzi wa Russia Serguei Choigou amesema katika taarifa “Kwa jumla, wanajeshi 71 waliuawa na wengine 210 kujeruhiwa kati ya wanajeshi waliokuwa na jukumu la kujibu mashambulizi ya adui.”

Choigou ameripoti pia vifaru 15 na magari tisa ya kivita yaliyoharibiwa.

Amesema Ukraine ilitumia idadi kubwa ya vifaa na wanajeshi kwenye maeneo tofauti ya mapambano tangu siku ya Jumapili na ilipata pia hasara katika mashambulizi hayo.

“Majaribio ya mashambulizi yalizimwa, adui hakufikia malengo yake, alipata hasara kubwa,” waziri Choigou ameongeza.

Russia ilithibitisha tangu Jumatatu kwamba ilizima mashambulizi makali ya Ukraine, ikimaanisha kuwa yalikuwa mashambulizi dhidi ya Russia yaliyokuwa yamepangwa na Kyiv tangu miezi kadhaa iliyopita.

Lakini Ukraine ilipuuza taarifa kuhusu mapigano hayo, ikidai hata hivyo siku ya Jumatatu kuteka tena maeneo kadhaa karibu na mji wa Bakhmut, ambao ni kitovu cha mapigano hayo.

Forum

XS
SM
MD
LG