Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Mei 26, 2024 Local time: 11:12

Will Smith apigwa marufuku kushiriki Oscars kwa miaka 10


Will Smith akilia wakati akipokea tuzo ya Oscars. Picha na AP/Chris Pizzello).
Will Smith akilia wakati akipokea tuzo ya Oscars. Picha na AP/Chris Pizzello).

Will Smith amepigwa marufuku kushiriki katika Oscars and matukio mengine ya Academy kwa miaka 10 baada ya kumchapa kibao muigizaji na mchekeshaji Chris Rock wakati wa hafla ya Oscars.

Academy of Motion Picture Arts and Science ambayo huandaa sherehe za kutoa tuzo, ilikuwa kwa njia ya mtanda Ijumaa kujadili hatua za kinidhamu. Smith aliomba msamaha kwa vitendo vyake na kujiuzulu kutoka Academy.

Smith alimchapa kibao Rock kwa kumfanyia utani mke wake ambaye alikuwa amekata nywele, ikiwa ni kutokana na hali ya kiafya ya ugonjwa unaojulikana kama alopecia ambao humfanya mtu kunyonyoka nywele.

Chini ya saa moja baadaye, alipewa tuzo ya muigizaji bora kwa uigizaji wakati kama “King Richard,” ambapo aliigiza kama baba wa nyota wawili wa tennis Venus na Serena Williams.

Katika taarifa yake, Academy ilisema kuwa Oscars “iligubikwa na tabia mbaya na isiyokubalika hata kidogo ambayo Bwana Smith aliionyesha jukwaani.”

Will Smith, kulia, ampiga kibao cha usoni Chris Rock akiwa jukwaani katika sherehe za kukabidhi tuzo za Oscars, March 27, 2022, Los Angeles.(AP Photo/Chris Pizzello)
Will Smith, kulia, ampiga kibao cha usoni Chris Rock akiwa jukwaani katika sherehe za kukabidhi tuzo za Oscars, March 27, 2022, Los Angeles.(AP Photo/Chris Pizzello)

Katika taarifa yake ya kujiuzulu, Smith alisema “amesaliti uaminifu wa Academy” na alikuwa :”amevunjika moyo” kwa vitendo vyake. Aliongezea kuwa “atakubali kikamilifu hatua yoyote itakayochukuliwa kutokana na vitendo vyangu.”

Kujiuzulu kwake kuna maana kuwa hataweza kupiga kura kwa Oscars siku zote. Tathmini ya nidhamu ya Academy juu ya tukio hilo, awali ilitarajiwa kufanyika Aprili 18, lakini iliharakishwa baada ya Smith kujiuzulu.

Wachache wameshawahi kujiuzulu kutoka Academy. Wanachama wanne – mzalishaji Harvey Weinstein, muigizaji Bill Cosby, muelekezi Roman Polanski na muigizaji sinema Adam Kimmel – waliondolewa kutokana na shutuma za vitengo vya ngono, wakati muigizaji Carmine Caridi alifukuzwa mwaka 2004 kwa kuzifanyia biashara video ambazo alipewa.

Lakini viwango vya utendaji vilivyowekwa na Academy vilihusu hatua kadhaa za kinidhamu kwa Smith, kama vile kuenguliwa kushiriki katika sherehe za Oscars, kumfutia uhalali wake wa kupewa tuzo au kuichukua tuzo aliyoshinda katika Oscar.

Ni tuzo moja tu ya Oscar imechukuliwa; ya filamu iliyoitwa “Young Americans” ambayo ilikuwa documentari nzuri mwaka 1969 lakini iligundilikwa kuwa haikustahili kwa tuzo mwaka huo.

Whoppi Goldberg (REUTERS/Eduardo Munoz - RC172B7A2F80
Whoppi Goldberg (REUTERS/Eduardo Munoz - RC172B7A2F80

Mwishoni mwa mwezi uliopita, muigizaji Whoopi Goldberg – mwanachama wa bodi ya gavana ya academy – alibashiri Smith huenda akakabiliwa na “adhabu kali” lakini alisema “lakini hatutaichukua tuzo yake ya Oscar.”

Mbali na hatua ya Academy, studio mbili – Sony and Netflix – zimesimamisha miradi yao na Smith.

Rock, ambaye hivi karibuni alifanya kazi yake ya uchekeshaji muda mfupi baada ya tukio la Oscars, hajatoa maoni yoyote hadharani kuhusu kuchapwa kibao.

Aliwaambia mashabiki wake katika show mwezi uliopita kwamba “Bado anatafakari kile kilichomtokea” na atazungumzia tukio hilo “wakati fulani.”

XS
SM
MD
LG