Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Septemba 22, 2023 Local time: 19:09

Hollywood: Filamu 'The Shape of Water' yanyakuwa tuzo nne za Oscars


Lupita Nyong'o, Winston Duke na Danai Gurira (kuanzia kushoto) wakiwasili katika maonyesho ya tuzo za Oscars huko Hollywood, jimbo la California., Machi 4, 2018.

Filamu ya kufikirika inayoitwa The Shape of Water (maumbile ya maji) imepata zawadi nne za Oscars wakati wa kutolewa tuzo za Academy siku ya Jumapili jioni, ikiwemo katika kundi la picha bora.

Filamu hiyo imempa nafasi mkurugenzi mwenye asili ya Mexico Guillermo del Toro kupata zawadi ya mkurugenzi wa filamu bora na pia kupata heshima kwa tathmini ya awali na uzalishaji wenye ubunifu.

Mwandishi wa VOA ameripoti kutoka mji wa Los Angeles ambapo onyesho hilo la Oscar lilifanyika maudhui ya usawa kwa wote yametawalia tuzo katika mwaka ambao wengi huko Hollywood wameungana kuwatetea wanawake.

Frances McDormand alitajwa kuwa muigizaji bora wa kike katika nafasi yake kama mama ambaye katika filamu hiyo alikuwa tayari kumumbua mkuu wa polisi katika juhudi zake za kutaka kumbainisha mtu aliyehusika na muuaji wa mtoto wake wa kike katika filamu maarufu Three Billboards Outside Ebbing, Missouri.

Swali ambalo wapenzi wengi wa filamu walikuwa wanajiuliza iwapo yoyote katika washindi wa tuzo ya Oscar mwaka 2018, jana Jumapili huko Hollywood, California, atatumia hotuba yake ya kupokea tuzo hiyo kuendeleza ajenda ya kisiasa, mtu pekee wa kumshukuru - au kumlaumu – Marlon Brando.

Wakati akipokea tuzo hiyo ya Oscar jana Jumapili, McDormand aliwaomba wanawake wenzie wasimame akiwemo mwigizaji mwanamke Meryl Streep.

“Waigizaji –Meryl, ukisimama, wengine wote watasimama, haya basi fanyeni hivyo – waongozaji wa filamu, wazalishaji wa filamu, wakurugenzi, waandishi wa filamu, Wakurugenzi wa picha, watengenezaji wa nyimbo, wandishi wa nyimbo, wabunifu.”

Amesema kuwa kila moja kati ya wanawake hao anajambo la kusimulia na mradi ambao unahitaji ufadhili.

Historia inaonyesha kuwa muigizaji wa Vito Corleone mwaka 1972 katika filamu The Godfather bado ni mashuhuri sana na mwenye kukonga nyoyo za wengi katika tasnia ya filamu.

Lakini kitendo chake cha kuingiza siasa mwaka 1973 wakati wa kupokea tuzo ya Academy Awards kilibadilisha mwenendo mzima wa Oscar.

Utamaduni uliokuwepo wakati huo ni washindi wa Oscar walipokea tuzo zao na kutoa hotuba wakiishukuru taasisi hiyo na sekta ya filamu.

Lakini Brando alileta mabadiliko. Yeye hata hakuhudhuria tafrija hiyo ya Oscar. Alimtuma mwigizaji Sacheen Littlefeather kumwakilisha. Alizungumza kupinga namna Hollywood ilivyokuwa inawafanyia watu ambao ni Wazawa wa Marekani (Native Americans).

Siasa zilijitokeza kuonyesha kuwepo athari za Brando katika sherehe za tasnia hiyo.

Maudhui yaliyojikariri wakati wa hafla hiyo jioni: madai ya unyanyasaji wa ngono na hoja dhidi ya kuongezeka idadi ya wanaume Hollywood. Pia tajiri katika ulimwengu wa filamu Harvey Weinstein, ambaye amekuwa akikabiliwa na tuhuma lukuki, amezuiwa kushiriki katika kinyang’anyiro cha maonyesho ya academy yaliyofanyika Oktoba.

Wengi waliohudhuria maonyesho hayo walivaa nguo nyeusi na beji nyeupe zenye ujumbe Time’s Up movement, ambayo ni umoja wa wanaharakati wanaotoa msaada wa kisheria kwa wanawake waliokuwa wamenyanyaswa kijinsia katika maeneo ya kazi.

Wengine walikuwa wamevaa riboni za rangi ya machungwa na beji zinazotaka hatua zichukuliwe dhidi ya matumizi mabaya ya silaha katika uvunjifu wa amani, kufuatia vifo vya watu 17 katika shule ya sekondari jimbo la Florida.

Maudhui nyingine katika maonyesho hayo jioni: Nguvu ya filamu katika kuleta mabadiliko katika jamii. Wakati akipokea tuzo ya Oscar kwa kuwa muongozaji wa filamu bora, del Toro amesema filamu zinaondoa vizuizi kati ya jamii.

XS
SM
MD
LG