Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Februari 26, 2024 Local time: 10:01

Oscars: Smith ampiga Rock kibao, akerwa na utani ulioelekezwa kwa mkewe


Will Smith, akimpiga mchekeshaji Chris Rock usoni (Foto AP/Chris Pizzello)
Will Smith, akimpiga mchekeshaji Chris Rock usoni (Foto AP/Chris Pizzello)

Mshindi wa tuzo ya mwigizaji bora mwanaume katika hafla ya Oscars ya mwaka 2022, Will Smith, alimpiga mchekeshaji Chris Rock usoni na kumtolea maneno machafu kwa kufanya mzaha kuhusu mtindo wa nywele wa mkewe.

Kisa hicho kinatajwa kama cha kushangaza, na ambacho kimekuwa gumzo kuu, kuhusiana na tuzo hizo za jana Jumapili.

Baadaye, wakati akipokea Oscar yake ya kwanza kama mwigizaji bora kwa nafasi yake katika "King Richard," Smith aliomba msamaha kwa waandaaji wa tamasha hilo, Oscars Academy, na wateule wenzake katika hotuba iliyojaa machozi, lakini si kwa muigizaji Chris Rock.

Matukio mengine yaliyovutia ni pamoja na onyesho la ufunguzi la mwanamuziki Beyonce, ushindi wa Ariana DeBose, kama muigizaji msaidizi bora zaidi, muda wa ukimya kwa watu wa Ukraine, na wimbo wa "We Don't Talk About Bruno."

Tuzo ya picha bora zaidi ilienda kwa filamu ya CODA, kuhusu familia ya watu wenye changamoto za kusikia.

XS
SM
MD
LG