Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Machi 25, 2023 Local time: 17:08

WB yasitisha mkopo wa Dola milioni 300 kwa Tanzania


Rais John Magufuli

Benki ya Dunia (WB) imesitisha mkopo wa elimu wa Dola za Marekani milioni 300 uliokuwa utolewe Tanzania kutokana na sera ya nchi hiyo inayokataza wasichana wajawazito kuendelea na masomo.

Programu hiyo ya Dola milioni 300 ilikuwa inakusudia kuisaidia Wizara ya Elimu nchini Tanzania kuweza kuboresha kupatikana kwa elimu ya sekondari yenye viwango.

Ilikuwa tayari imepangwa mkopo huu uidhinishwe na uongozi wa benki hiyo mwishoni mwa mwezi Octoba. Lakini chanzo cha habari ndani ya benki hiyo imeiambia CNN mradi huo badala yake ulikuwa umeondolewa na hautatekelezwa tena.

Sera ya Tanzania ya kuwafukuza wanafunzi wenye ujauzito mashuleni ni moja ya sababu ya mkopo huo kuondolewa, chanzo cha habari kimesema.

Sheria hiyo ilikuwepo tangu mwaka 1960, lakini imekuwa sasa ikitekelezwa zaidi baada ya Rais John Pombe Magufuli alipochukuwa madaraka 2015.

Juni iliyopita, Magufuli ambaye alipewa jina la “Tingatinga,” alichukuwa hatua zaidi, kutangaza kuwa wanafunzi wajawazito hawataruhusiwa kurejea mashuleni baada ya kujifungua.

Wanafunzi hao walichukuliwa vipimo vya ujauzito na kuonekana wana mimba shuleni. Baada ya hapo wakafukuzwa.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG