Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Oktoba 25, 2020 Local time: 03:01

Mahakama yamwachia Abdul Nondo baada ya kukosekana ushahidi


Abdul Nondo wapili kulia akiwa mahakamani baada ya kuachiwa huru.

Mahakama ya Hakimu Mkazi Iringa, Tanzania imemuachia huru Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi (TSNP), Abdul Nondo, Jumatatu, Novemba 5, 2018, baada ya upande wa mashitaka kushindwa kuthibitisha makosa alioshtakiwa kwayo.

Katika kesi hiyo ambayo Nondo alikuwa akikabiliwa na makosa mawili ya kudanganya kutekwa na kutoa taarifa za uongo, mahakama hiyo imemkuta hana hatia baada ya upande wa Jamhuri kushindwa kueleza mshitakiwa alifikaje Mafinga.

Shirika la habari la Global Publishers aidha limeripoti kuwa mahakama imesema hakuna ushahidi kutoka upande wa Jamhuri kuwa mshitakiwa alikuwa wapi wakati wa tukio na kuifanya kesi hiyo ikose ushahidi.

Kwa mujibu wa upande wa utetezi imebainika kuwa upande wa mashtaka wametoa ushahidi wa hisia na hivyo mahakama kuamua kumuachia huru.

Facebook Forum

Kura ya Maoni : Uchaguzi Tanzania

Kama unapiga kura leo utampigia nani kura yako ya urais?

Kura hii ya maoni si ya kisayansi na inaonyesha maoni ya waliojibu maswali tu.

Kama unapiga kura leo utampigia nani kura yako ya urais?

Kura hii ya maoni si ya kisayansi na inaonyesha maoni ya waliojibu maswali tu.

XS
SM
MD
LG