Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Machi 19, 2024 Local time: 05:35

Amnesty International yataka serikali imdhibiti Makonda


Nembo ya Amnesty International
Nembo ya Amnesty International

Tangazo la mipango ya kuunda kikosi kazi ambacho kitaanza kuwasaka na kuwakamata watu ambao wanadhaniwa kuwa ni mashoga, au watu wa jinsia moja wenye mahusiano ya kimapenzi, kuanzia wiki ijayo, limezua taharuki katika jumuiya ya kimataifa.

Mkurugenzi wa shirika linalotetea haki za binadamu, Amnesty International, katika kanda ya Afrika Mashariki, Pembe ya Afrika na nchi za Maziwa Makuu Joan Nyanyuki ameiambia Sauti ya Amerika mkakati mzima wa kuwepo kikosi kazi ni lazima usitishwe mara moja kwani unachangia kuhamasisha chuki kati ya wananchi.

Mkurugenzi huyo amesisitiza kuwa: "Ni jambo la kusikitisha kuwa Tanzania imechagua kuchukua hatua hii hatari katika kukishughulikia kikundi ambacho tayari ni watu waliotengwa."

Amesema Suala la kikosi kazi ni lazima lisitishwe mara moja kwani linachangia katika kuhamasisha chuki kati ya wanajamii. Mashoga tayari wanakabiliwa na ubaguzi, vitisho na kushambuliwa bila ya kuwepo matamko ya chuki ya aina hii.

“Serikali ya Tanzania lazima ihakikishe kuwa hapana mtu yoyote, hasa wale walioko katika madaraka kama vile Paul Makonda, anatoa matamko au anachukuwa hatua kupandikiza chuki ambazo zinahatarisha maisha ya watu kwa sababu tu ya jinsia yao au maumbile yao.

Hivyo basi serikali inalojukumu la kumlinda kila mtu nchini Tanzania na kuheshimu haki zao za kibinadamu bila ya kuwabagua.

“Serikali inajukumu la kumlinda kila mtu nchini Tanzania na kuheshimu haki zao za kibinadamu bila ya kuwabagua. Ni lazima ichukue jukumu hili kwa uzito mkubwa na isianzishe programu au kutumia vyombo vya dola kuwaibia watu wa jinsia moja wenye mahusiano haki zao.

XS
SM
MD
LG