Makubaliano hayo yalifikiwa Dubai baada ya wiki mbili za mashauriano magumu ambayo yalitarajiwa kutuma ishara yenye nguvu kwa wawekezaji na watunga sera kwamba dunia inaungana katika lengo lake la kuachana na mafuta ghafi jambo ambalo wanasayansi wanasema ni tumaini bora la kupambana na janga la hali ya hewa.
Rais wa COP28 Sultan Al Jaber ameuita mpango huo kuwa ni wa kihistoria. lakini akaongeza kuwa mafanikio yake yatakuwa katika utekelezaji wake.
“wakati wa usiku na mapema asubuhi, tulifanya kazi kwa pamoja kufikia muafaka. Uraisualisikiliza, ulishiriki na kuongoza. Ninaahidi nitajitahidi sana na nitakuwa pamoja nanyi katika kila hatua. Na nyinyi, wafanyakazi wenzangu na marafiki, mmejitokeza haswa, mmeonyesha mnaweza kubadilika, na kueka maslahi ya pamoja mbele badala ya maslahi binafsi.” Alisema Rais hyo wa COP28.
Aliongeza kwa kusema “Tumekabiliana na hali halisi na tumeiweka dunia katika mwelekeo sahihi. Tumeipatia mpango thabiti wa utekelezaji ili kufikia kiwango cha 1.5. ni mpango unaoongozwa na sayansi. Ni mpango wa usawa ambao unakabiliana na uzalishaji , kuziba mwanya na kutekeleza , kufikiria upya ufadhili wa kimataifa na kuondoa hasara na uharibifu.
Zaidi ya nchi 100 zimekuwa zikifanya ushawishi mkubwa katika makubaliano ya COP28 ili kuondoa matumizi ya mafuta , gesi makaa ya mawe lakini zilipinga upinzani mkali kutoka kundi la wazalishaji mafuta linaloongozwa na Saudi Arabia OPEC ambalo lilisema kuwa ulimwengu unaweza kuondoa hewa chafu bila kuachana na mafuta.
Forum