Masuala yenye utata ni pamoja na makubaliano kuhusu matumizi ya mafuta ya ghafi, yanayotajwa kuwa sababu moja wapo ya kuongeza kiwango cha joto duniani. Wanaharakati mapema Jumanne wamekusanyika karibu na ukumbi wa mkutano, wakiendelea na malalamiko yao ya kutaka kusitishwa matumizi ya mafuta ghafi, ufadhili kamili wa umma, uungaji mkono wa kijinsia, pamoja na haki za biinadamu.
Mmoja wa watu walioandamana Sebastien Duyck kutoka kituo cha kimataifa cha sheria za kimazingira, amesema kwamba anatarajia kuwa mataifa yalioendelea yatatimiza ahadi zao za kutoa fedha kwa ajili ya utunzaji wa mazingira. Mazungmzo hayo yalitarajiwa kumalizika Jumanne, lakini mara nyingi huwa yanachukua muda mrefu kutokana na washiriki kutokubaliana.
Forum