Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Januari 19, 2025 Local time: 06:36

Mkuu wa UN katika mkutano wa hali ya hewa ayashinikiza mataifa kufikia makubaliano na kuondoa tofauti zao


Rais wa COP28, Sultan Ahmed Al Jaber. Picha na KARIM SAHIB / AFP
Rais wa COP28, Sultan Ahmed Al Jaber. Picha na KARIM SAHIB / AFP

Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika mkutano wa hali ya hewa ameyashinikiza mataifa  Ijumaa kufikia makubaliano wakati mazungumzo yakianza tena, huku zikiwa zimebaki siku nne tu kwa mashauriano kuondoa tofauti zao juu ya hatima ya vyanzo vya asili vya nishati.

Wakati mazungumzo ya Umoja wa Mataifa ni nadra kumalizika kwa wakati, rais wa COP28 Sultan Al Jaber ameweka matarajio ya lengo ya kuhitimisha mkutano wa huko Dubai uwe ni saa tano asubuhi kwa saa huko siku ya Jumanne.

Wanaharakati kutoka Mashirika yasiyo ya kiserikali likiwemo Fridays For Futuru yanapinga pembeni ya mazungumzo ya hali ya hewa ya Umoja wa Mataifa ya COP28 mjini Dubai, yakidai haki kwa hali ya hewa na kumalizwa kwa vyanzo vya asili vya nishati.

Huku dunia ikikabiliwa na mwaka wenye joto kali sana na mioto ya msituni na mafuriko ambayo yamezipiga jamii kote ulimenguni, wapatanishi katika mazungumzo ya COP28 ambapo Umoja wa Falme za Kiarabu yenye utajiri wa mafuta kama mwenyeji iko katika shinikizo la kusimamia kupitishwa kwa makubaliano ya kihistoria kuhusu vyanzo vya asili vya nishati.

Vanessa Nakate, Mwanaharakati wa Haki kwa Hali ya Hewa, Uganda na Balozi wa Hisani wa UNICEF anaeleza: “Viongozi hapa Dubai wana fursa ya kihistoria, lazima watekeleze digirii 1.5 za Celsius wakati rais wa COP28 Al Jaber amerejea utoa wito na kutangaza kupunguza kwa kiwango kidogo tu cha nishati ya asili."

Huku mawaziri hivi sasa wako mjini kutekeleza makubaliano, Jaber amesema anawataka wapatanishi kuja na rasimu mpya ya makubaliano ya Ijumaa.

Sultan Al Jaber, Rais wa COP28 anasema: “Ni muhimu kwamba tubadili mwelekeo na kwamba tuwapate mawaziri na wakuu wa ujumbe kujihusisha katika kile nyanja ya GST.”

Licha ya kutokukubaliana juu ya mustakbali wa vyanzo vya asili vya nishati, Jaber ameelezea imani yake kwamba mazungumzo ambayo Umoja wa Falme za Kiarabu yenye utajiri wa mafuta ni mwenyeji unaweza kumalizika kwa makubaliano ya kihsitoria.

Habari hii inatokana na vyanzo mbalimbali vya habari.

Forum

XS
SM
MD
LG