Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Mei 11, 2024 Local time: 21:20

Watu 47 wamefariki kufuatia mafuriko katika mkoa wa Manyara nchini Tanzania


Mafuriko yanayoendelea nchini Tanzania
Mafuriko yanayoendelea nchini Tanzania

Watu wasiopungua 47 wamefariki na 85 wengine wamejeruhiwa kutokana na mafuriko katika mkoa wa Manyara huko kaskazini mwa Tanzania kutokana na mvua kubwa iliyosababishwa na hali ya hewa ya El Nino.

Mkuu wa mkoa wa Manyara, Queen Sendiga amesema mpaka majira ya saa 10 jioni kwa saa za Afrika Mashariki siku ya Jumapili vifo vilifikia idadi hiyo ambapo pia kulikuwa na uharibifu wa mali za watu wilayani humo.

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan
Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan

Wakati huo huo Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akiwa mjini Dubai akihudhuria mkutano wa mabadiliko ya hali ya hewa COP28, alitoa salamu za rambirambi kwa njia ya video akiwapa pole wale walioathiriwa na maafa hayo katika kipindi hiki cha mvua za El Nino zinazoendelea kunyesha katika ukanda mzima wa Afrika Mashariki. Mvua hiyo ilisababisha sehemu ya mlima Hanang kumomonyoka na kusababisha tope kubwa kutiririka katika maeneo ya Katesh na Gendabi.

VOA imezungumza na mwandishi wa kujitegemea Deo kaji Makomba akiwa Dodoma na kwanza kutaka kujua serikali imetoa tamko gani kuhusiana na tukio hili na nini kinachofanyika kwa waathiriwa.

Mwandishi Deo Makomba akizungumza na VOA Kumekucha.m4a
please wait

No media source currently available

0:00 0:03:01 0:00

Forum

XS
SM
MD
LG