Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Oktoba 08, 2024 Local time: 08:23

Mjadawa wa nishati mbadala ya mafuta bado kitendawili COP28


Wapatanishi katika mkutano wa hali ya hewa wa COP28, mjini Dubai, Jumapili hawajafikia muafaka juu ya hali ya baadaye kwa nishati ya vyanzo vya asili wakati mazungumzo katika mkutano yakiingia katika hatua za mwisho.

Shauri la iwapo dunia inapaswa kwa mara ya kwanza kabisa kukubaliana kumaliza enzi za matumizi ya nishati ya mafuta limekuwa kiini cha mkutano huo wa kimataifa ambapo takribani nchi 200 zinajaribu kufikia muafaka wa mabadiliko ya hali ya hewa.

Muungano wa zaidi ya nchi 80 zikiwemo Marekani, Umoja wa Ulaya, na mataifa ya visiwa vidogo ulishinikiza makubaliano ambayo yanajumuisha msimamo wa kuondoa mafuta, gesi, na makaa ya mawe kama nishati za msingi lakini walikabiliwa na upinzani mkali unaoongozwa na kundi la wazalishaji mafuta OPEC na washirika wake.

Forum

XS
SM
MD
LG