Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Julai 14, 2024 Local time: 08:00

Watu zaidi ya 12 wauawa DRC

Nyumba za wananchi walioshambuliwa na kuuawa katika kijiji cha Masome, mjini Komanda ,DRC, zikiwa hazina milango baada ya watu zaidi ya 12 kuuawa, hivyo familia zimekimbia makazi yao. Picha na Mwandishi wa VOA Austere Malivika, Mkoani Ituri, DRC.

Watu zaidi ya 12 wameuwawa katika kijiji cha Masome kilomita nane kutoka Mji wa Komanda uliopo kilometa hamsini na saba kutoka mji wa Bunia Mkoani Ituri.

Kiongozi wa kata ya Komanda aliyejitambulisha kwa jina moja la Makayanga amesema mili ya watu 10 na miwili imepatikana, wote ni wakulima ambao walifungwa kamba mikononi wakiwa na alama ya kudungwa visu na wengine kukatwa kwa mapanga.

Makayanga amesema watu hao walikuwa katika shamba lao wakilima kahawa na kakao kwa bahati mbaya walizingirwa na watu wasiojulikana walio kuwa na mapanga na kuanza kuwauwa baada ya kuwafunga mikono na hata kuwateka wengine hadi porini.

Eneo la Komanda lililopo katika mkoa wa Ituri karibu na eneo la Kivu Kaskazini limekuwa likishuhudia mauaji na machafuko kwa muda mrefu na hivyo kuwalazimisha wakaazi wa eneo hilo kuhama nyumba zao na kukimbilia sehemu zenye usalama.

Nyumba za wananchi walioshambuliwa na kuuawa katika kijiji cha Masome, mjini Komanda ,DRC, zikiwa hazina milango baada ya watu zaidi ya 12 kuuawa, hivyo familia zimekimbia makazi yao. Picha na Mwandishi wa VOA Austere Malivika, Mkoani Ituri, DRC.
Nyumba za wananchi walioshambuliwa na kuuawa katika kijiji cha Masome, mjini Komanda ,DRC, zikiwa hazina milango baada ya watu zaidi ya 12 kuuawa, hivyo familia zimekimbia makazi yao. Picha na Mwandishi wa VOA Austere Malivika, Mkoani Ituri, DRC.

Wakati huohuo wafanya biashara katika mji wa Butembo katika jimbo la Kivu Kaskazini mashariki mwa DRC wanaendelea na mgomo wakufunga maduka kutokana ukosefu wa usalama wilayani Beni, Lubero na mkoani Ituri.

Tshongo Patrick mfanya biashara katika mji wa Butembo, ni mmoja waliogoma kufungua maduka yao akisema wameitisha mgomo na kufunga shughuli zote za biashara mjini humo kwa sababu serikali imekaa kimya wakati watu wanapitia mateso huku malori na magari yao yakichomwa kila siku na watu wanao dhaniwa kuwa waasi wa kikundi la ADF katika barabara ya Beni Kasindi na Beni Bunia.

Biashara zimefungwa mjini Butembo kutokana na waasi wa ADF kushambulia wananchi, kuchoma malori na magari yao. Picha na Austere Malivika.
Biashara zimefungwa mjini Butembo kutokana na waasi wa ADF kushambulia wananchi, kuchoma malori na magari yao. Picha na Austere Malivika.

Mbusa Eugene kwa upande wake amesema wapo tayari kuendelea kulipa kodi kwa masharti kwamba serikali iwape ulinzi na kukomesha mauaji.

Wachambuzi wanasema mgomo huo unasababisha serikali kutofaidika na hata wafanya biashara wenyewe nao kupoteza kipato chao.

jeshi la Wananchi la DRC likishirikiana na Jeshi la Wananchi la Uganda linafanya operesheni maalum kupambana na waasi katika eneo la Beni, DRC. Picha na mwandishi wa VOA Austere Malivika.
jeshi la Wananchi la DRC likishirikiana na Jeshi la Wananchi la Uganda linafanya operesheni maalum kupambana na waasi katika eneo la Beni, DRC. Picha na mwandishi wa VOA Austere Malivika.

Wanananchi nchini DRC wanaomba kuhakikishiwa usalama wao kufuatia ahadi za serikali za kuimarisha ulinzi inazozitoa mara kwa mara.

Imetayarishwa na mwandishi wetu Austere Malivika, Goma, DRC.

XS
SM
MD
LG