Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 27, 2024 Local time: 04:17

Watu wasiopungua 30 wafariki katika mfululizo wa ajali za boti zilizobeba wahamiaji Ugiriki


Ramani ya Bahari ya Aegean, Greece.
Ramani ya Bahari ya Aegean, Greece.

Walinzi wa pwani wa Ugiiki walijitahidi kuwaokoa manusura katika bahari ya Aegean Jumamosi baada ya mfululizo wa ajali za boti zilizobeba wahamiaji ambazo zimeua takriban watu 30 katika muda wa siku chache.

Ijumaa jioni, walinzi wa pwani walipata miili 16, ikiwemo miili ya wanawake watatu na mtoto mmoja, na kuwaokoa watu 63 kutoka kwenye boti iliyopinduka na kuzama karibu na kisiwa cha Paros.

Kwa mujibu wa wale waliookolewa, kiasi cha watu 80 walikuwa ndani ya boti hiyo.

Boti tatu za walinzi wa pwani, boti binafsi, na ndege ya ulinzi wa pwani pamoja na wazamiaji walikuwa wanawasaka manusura zaidi, maafisa wamesema.

Janga la karibuni – la tatu tangu Jumatano – limekuja wakati harakati za magendo hazijaonekana kwa miezi kadhaa katika maji ya Ugiriki.

Wakimbizi na wahamiaji akiwasili katika boti zilizofurika katika kisiwa cha Lesbos, Ugiriki, November 10, 2015.
Wakimbizi na wahamiaji akiwasili katika boti zilizofurika katika kisiwa cha Lesbos, Ugiriki, November 10, 2015.

Saa kadhaa awali, miili 11 ilipatikana kutoka kwenye boti nyingine ambayo ilizama kwenye eneo la kaskazini mwa kisiwa cha Ugiriki cha Antikythera siku ya Alhamisi jioni.

Watu 90 waliokwama kisiwani waliokolewa, walinzi wa pwani walisema.

Jumatano, boti moja chakavu iliyobeba wahamiaji ilipinduka karibu na kisiwa cha Folegandros, na kuua watu watatu.

Watu 13 waliokolewa, wakazi dazeni bado hawajapatikana, maafisa wa Ugiriki walisema.

Manusura walitoa habari zakukanganya: baadhi wakisema kulikuwa na watu 32 kwenye boti na wengine wakitaja idadi kufikia watu kiasi cha 50, mlinzi mmoja wa pwani ameliambia shirika la habari la AFP.

Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi *UNHCR) limesema ajali ya Folegandros huenda ikawa ni ajali mbaya huko Aegean mwaka huu, idadi ya isiyojulikana ya watu bado wamepotea.

“Mabaki ya boti ni ukumbusho wenye maumivu ambao watu wanaendelea panda boti na kusafiri kwenye njia hatari ambayo si salama,” alisema Adriano Silvestri, mwakilishi msaidizi wa UNHCR nchini Ugiriki.

Mapema Ijumaa, walinzi wa pwani waliingilia kati boti nyingine iliyokuwa na wanaume 92 na wavulana baada ya kukwama kwenye ufukwa wa peninsula ya Peloponnese.

Washukiwa wafanya magendo watatu ambao walikimbia na kuiacha boti walikamatwa baadaye.

UNHCR inakadiria kwamba zaidi ya watu 2,500 wamefariki au kupotea baharini wakati wakijarbu kufika Ulaya kuanzia Januari mpaka Novemba mwaka huu.

Takriban watu milioni moja, wengi wao wakimbzi kutoka Syria, waliwasili Umoja wa Ulaya mwaka 2015 baada ya kuvuka bahari ya kwenye visiwa vya Ugiriki karibu na Uturuki.

“Siku hizi, harakati za wafanya magendo, ambao hawajali maisha ya binadamu, zimeongezeka, na kuwarubuni watu wenye shida, bila ya kuwapatia majaketi ya kuokoa maisha, kwenye boti ambazo hazina hata vigezo vya kawaida vya usalama,” Gianis Plakiotaki, waziri wa masuala ya baharini amesema Ijumaa jioni akiinyooshea kidole Uturuki, akisema Ankara, “inaruhusu wafanya magendo bila ya kuwakagua.”

Mahasimu Ugiriki na Uturuki kila mara wanashutumiana juu ya suala la wahamiaji, huku Athens ikiishutumu Ankara kwa kufumbia macho watu wanaojaribu kuvuka kuingia katika nchi mwanachama wa EU, Ugiriki na Uturuki imekanusha shutuma hizo.

Chanzo cha habari hii ni Shirika la Habari la AFP

XS
SM
MD
LG