Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 26, 2024 Local time: 18:39

Marekani, EU, Uingereza na Canada wawekea Belarus vikwazo


Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken amesema kwamba, EU , Uingereza na Canada wametangaza vikwazo vipya kwa maafisa wa Belarus pamoja na makampuni. 

Hatua hiyo ni kutokana na kile wametaja kuwa hujuma ya serikali dhidi ya demokrasia, ukiukaji wa haki za binadamu,kutoheshimu sheria za kimataifa pamoja na kukandamiza watu wa Belarus walioko ndani na nje ya nchi.

Marekani inalenga maafisa 32 pamoja na taasisi zikiwemo zile za serikali ambazo zinaunga mkono serikali ya rais Alexander Lukashenko. Mwana wa kiume wa Lukashenko, Dmitry pia ni miongoni mwa watu waliowekewa vikwazo.

Marekani pia imesitisha uwezo wa serikali ya Belarus wa kupata mikopo. Lukashenko amekuwa akiwasaka wapinzani wake wa kisiasa tangu kumalizika kwa uchaguzi wa 2020, ambao ulitajwa na Marekani na EU kuwa wenye udanganyifu.

Belarus pia inalaumiwa kwa kutumia wahamiaji kama silaha ya kisiasa dhidi ya majirani wake kama Poland. Vikwazo vya EU ni dhidi ya maafisa waliohusika kwenye sakata la wahamiaji pamoja na mashirika mawili ya ndege ya Belavia na Syrian airline Cham Wings, ambayo yanasemekana kuleta wahamiaji nchini Belarus ili kuvuruga hali zaidi.

XS
SM
MD
LG