Boti hiyo ilikuwa imewabeba Waindonesia 50 ili kuingia nchini Malaysia kinyume cha sheria.
Ajali hiyo ilitokea Jumatano wakati kuna hali mbaya ya hewa kusini mwa jimbo la Johor.
Idadi ya vifo ilipanda na kufikia 16 Alhamisi baada ya operesheni ya timu ya uokozi kupata miili mitano zaidi ya wahamiaji wa Indonesia kwenye ufukwe.
Wanajeshi waliokuwa wakifanya doria waligundua miili 11 kwenye ufukwe saa kadhaa baada ya ajali hiyo.
Miili ya wanaume watatu na wanawake wawili iligunduliwa Alhamisi, walinzi wa pwani wamesema.
Wahamiaji 20 bado hawajulikani walipo, na maafisa wamepeleka boti na helikopta kuwatafuta.