Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 18, 2024 Local time: 22:25

Tetemeko la ardhi latokea Indonesia


Mlima wa Sinabung kisiwani Sumatra, Indonesia.
Mlima wa Sinabung kisiwani Sumatra, Indonesia.

Idara ya kitaifa ya jiolojia ya Marekani imesema Jumatatu kwamba tetemeko la ardhi la kiwangocha 5.9 kwa kipimo cha rikta limetokea kwenye ufukwe wa kisiwa cha Indonesia cha Sumatra bila kutoa onyo la kutokea kwa Tsunami wala ripoti za uharibifu au maafa.

Kwa mujibu wa shirika la habari la AFP, tetemeko hilo limetokea baharini likiwa na kimo cha kilomita 6 takriban kilomita 255 kusini mwa mji wa Sinabang.

Indonesia hushuhudia matukio kama hayo mara kwa mara kutokana na ukaribu wake wa kile kinachotajwa kuwa ulingo wa moto kwenye bahari ya Pacific,unaoanzia Japan ukipitia kusini mashariki mwa Asia hadi kwenya bahari ya Pacific.

Mwezi Januari zaidi ya watu 100 walikufa huku maelfu wakiachwa bila makazi kutokana na tetemeko la ardhi la 6.2 kwa kipimo cha rikta kwenye kisiwa cha Sulawesi, wakati likifanya uharibifu mkubwa wa majengo na barabara kwenye mji wa Mamuju.

XS
SM
MD
LG