Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Juni 18, 2024 Local time: 12:22

Idadi ya vifo yaongezeka Indonesia kutokana na Volcano


Indonesia Volcano
Indonesia Volcano

Idadi ya vifo kutokana na mlipuko wa mlima wa Volcano kwenye kisiwa cha Java nchini Indonesia imeongezeka na kufikia watu 34.

Shughuli za uokoaji zinaendelea.

Mlima Semeru, katika wilaya ya Lumajang, mkoa wa Java mashariki, ulilipuka na kutoa jivu zito lililofika umbali wa mita 12,000 kuelekea angani, huku gesi na Lava ikitiririka kuelekea chini ya mlima baada ya mlipuko huo.

Barabara zote zilizo karibu na mlima huo zilifunikwa kwa jivu na matope, nyumba na magari vikiharibiwa.

Waokoaji wanakumbana na hali hatari katika sehemu hiyo, wakitafuta manusura katika mabaki ya mlipuko huo. Wamekuwa wakitumia mbwa wa kunusa katika oparesheni hiyo.

Milipuko mingine midogo midogo imekuwa ikitokea kwenye mlima huo tangu jumamosu na kutatiza shughuli za uokoaji.

Maafisa wamesema kwamba milipuko mingine midogo imetokea leo jumanne, ikirusha jivu umbali wa kilomita moja kuelekea angani.

XS
SM
MD
LG