Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 13:22

Watu wanne wauawa Comoro., saba wajeruhiwa


Viongozi wa upinzani Comoros wakiongoza maandamano Jumatano, Machi 27, 2019.
Viongozi wa upinzani Comoros wakiongoza maandamano Jumatano, Machi 27, 2019.

Watu wanne wanaripotiwa kuuawa na wengine 7 kujeruhiwa kutokana na mashambulio la bunduki kati ya wanajeshi watiifu wa Rais wa Comoro Azali Assoumani na waasi waliongozwa na naibu mkuu wa zamani wa majeshi.

Vyanzo vya habari nchini vimesema kuwa kiongozi huyo wa waasi Faisal Abdelsalam ameuawa katika mapigano hayo.

Hali inaripotiwa kuwa tulivu lakini kuna wasi wasi juu ya usalama miongoni mwa wananchi kufuatia ghasia zilizotokea baada ya kutangazwa matokeo ya uchaguzi wa rais yanayopingwa na upinzani.

Jela yavunjwa

Mashambulio yalianza wakati wa alasiri saa za Comoros pale kundi la watu wasiojulikana walipovamia jela kuu ya Moroni na kuwaachilia huru wafungwa wote akiwemo naibu mkuu wa zamani wa jeshi Faisal Abelsalam.

Walifuatana naye hadi kambi kuu ya kijeshi na makao makuu ya jeshi la Komoro hapo Kandaana na kuanzisha mashambulio yaliyodumu kwa saa mbili hivi na kuzusha wasi wasi mkubwa katika mji mkuu wa Moroni.

Mchambuzi wa masuala ya kisiasa mjini Moroni Mohamed Mshangama anasema haifahamiki hadi hivi sasa nini malengo ya mashambulio hayo na kwanini ni kundi dogo tu lililokwenda kushambulia kambi hiyo.

Mshangama amesema kuwa haijulikani kwa nini kundi la watu 7 lilikwenda kushambulia kambi yenye mamia ya wanajeshi.

"Inaaminika kundi hilo lilitarajia kupata msaada kutoka kwa wanajeshi walioko ndani ya kambi, ambao inasadikiwa kuwa baadhi yao walikuwa wameasi," amesema.

Tamko la serikali

Serikali hadi hivi sasa haijatowa taarifa yeyote kuhusu shambulizi hilo lililotokea wakati rais Assoumani Azali akiwa kisiwani Nzwani akiripotiwa anatembelea wafuasi wake kuwashukuru kwa kumchagua katika uchaguzi wa rais ulofanyika jumapili 24.

Duru za kuaminika zinaripoti kwamba huwenda kundi hilo lilikwenda kumachilia huru mgombea kiti cha rais Solilihi Mohamed anaefahamika kama Kampanyar aliyekamatwa na wanajeshi kabla ya shambulio hilo hii leo. Mwanajeshi huyo wa zamani aliyegeuka mwanasiasa aliyeuliwa na wagombea wengine 11 kuongoza serikali ya mpito hapo jana ili kupinga utawala wa Azali na huwenda ndio maana akakamatwa naasema Mshangama.

Maandamano ya wanawake

Kabla ya tukio hilo kundi la wanawake kutoka tabaka mbali mbali waliandamana hadi jingo la mahakama kuu ili kuwasilisha tangazo lao dhidi ya uchaguzi wa rais. Nailaabass ni moja wapo ya watayarishaji wa maandamano hayo anasema wanasikitishwa wanajeshi waliwatawanya walipofika mbele ya jengo.

Naila Abass amesema kuwa : "Tulitaka kueleza usikitifu wetu juu ya jinsi uchaguzi ulivyofanyika kulikuwepo na kasoro nyingi, kwa hivyo tulitayarisha waraka hiyo kuonesha malalamiko yetu na kuitaka mahakama kuu kufutilia mbali matokeo ya uchaguzi huo."

Baada ya uchaguzi

Tangu kufanyika uchaguzi Jumapili hadi hii leo kumekuwepo na maandamano na ghasia hadi kufikia hii leo na Mshangama anasema matukio hayo yote yatabadilisha muelekeo wa kisiasa nchini humo.

"Wasi wasi ukiwa unaendelea watu wanasubiri uwamuzi wa mahakama kuu ikiwa itaidhinisha matokeo ya uchaguzi au kuitikia wito wa wananchi wengi kufutilia mbali uchaguzi huo," amesema Mshangama.

Imetayarishwa na mwandishi wetu, Abdushakur Aboud, Washington, DC.

XS
SM
MD
LG