Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Desemba 14, 2024 Local time: 10:31

Milio ya risasi yarindima katika kambi kuu ya jeshi Comoros


Comoros
Comoros

Milio ya bunduki inaendelea kusikika katika kambi kuu ya kijeshi ya Comoros baada ya polisi kumkamata mmoja wa wagombea kiti cha rais aliyeshindwa Swalihi Mohamed..

Wachambuzi waliozungumza na Sauti ya Amerika wanasema milio ya bunduki katika kambi ya Kaandi inatokana na mgawanyiko uloanza kujitokeza katika jeshi la Comoros kutokana na jinsi uchaguzi ulivyofanyika na kumpatia ushindi Rais Azali Assoumani.

Hali hiyo yote imetokea baada ya wanawake 18 kukamatwa Alhamisi mjini Moroni wakati wa maandamano makubwa yaliyofanywa na wanawake kupinga ushindi wa Rais Azali Assoumani katika uchaguzi ulofanyika Jumapili iliyopita.

Wanawake hao walikuwa wanataka kuwasilisha ujumbe Mahakama Kuu kuonya kwamba hali ya kisiasa inatia wasiwasi mkubwa kutokana na jinsi serikali ilivyoandaa na kufanya uchaguzi wanaosema uligubikwa na kasoro na matatizo chungu nzima.

Mandamano hayo yaliyoitishwa na umoja wa vyama vya wanawake Comoros, yalitawanywa na maafisa wa polisi kama yale yaliyofanyika siku za nyuma baada ya kufanyika uchaguzi.

Katika tangazo lao wanawake wanaitaka mahakama kuu kufutilia mbali matokeo ya uchaguzi, ambayo yanatokana na hesabu za kura zilizofanyika kwa njia iliyokuwa haijafuata sheria.

Imetayarishwa na Mwandishi wetu, Abdushakur Aboud, Washington, DC.

XS
SM
MD
LG