Upatikanaji viungo

Alhamisi, Februari 29, 2024 Local time: 22:32

Wagombea wote wa kiti cha rais Comoro wadai ushindi


Wafuasi wa mgombea wa upinzani washerehkea ushindi Comoros 2016
Wafuasi wa mgombea wa upinzani washerehkea ushindi Comoros 2016

Zowezi la kuhesabu kura likiendelea katika visiwa vya Comoro kutokana na duru ya pili ya uchaguzi wa rais hapo Jumapili, wagombea wawili wa juu tayari wanadai ushindi.

Matokeo rasmi hayatajulikana katika muda wa siku mbili au tatu zijazo, lakini wachambuzi wanasema tayari kuna wasi wasi mkubwa ulotanda nchini humo juu ya nani mshindi kutokana na kwamba uchaguzi huo ulikua na ushindani mkubwa kati ya rais wa zamani Asoumani Azali na makamu rais wa serikali inayondoka madarakani Mohamed Ali Saleh.

Uchaguzi unaripotiwa ulifanyika kwa utulivu na amani kote nchini pakiwepo na matatizo kadhaa katika visiwa vya Nzwani na Mwali, ambayo yaliweza kutanzuliwa na upigaji kura kuendelea.

Kufikia usiku wa manane saa za Afrika Mashariki matokeo ya awali yalianza kutokewa na rais wa zamani Asoumani Azali alionekana akiongoza katika visiwa vya Mwali na Nzwani huko kisiwa kikuu cha Ngazija kilikua baado kinahesabu kura zake.

Kufuatia malalamiko yaliyotokea katika duru ya kwanza ambapo upinzani walitaka kura kuhesabiwa tena kura, tume ya uchaguzi iliamua kwamba wagombea watakua na wajumbe wao katika kila kituo na kura kuhesabiwa katika vituo hivyo vya uchaguzi kabla ya kuwasilishwa makao makuu katika mji mkuu wa Moroni.

Wakomoro wengi wanataka mageuzi baada ya zaidi ya miaka minane ya utawala wa mungano wa vyama vya utawala unaongozwa na Mohamed Ali Solihi maarufu kama Mamadou.

Mgombea kiti cha rais Comoros Mohamed Ali Soilihi
Mgombea kiti cha rais Comoros Mohamed Ali Soilihi

Baadhi ya wapigakura walozungumza na Sauti ya Amerika wanasema ingawa hawamini upinzani utaweza kuleta mabadiliko lakini wana hisi itakua bora kubadili utawala na kuupatia upinzani unaoongozwa na Azali aliyechukua madaraka kwa mara ya kwanza kupitia mapinduzi 1999 na kuondolewa kwa uchaguzi 2006..

XS
SM
MD
LG