Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Januari 30, 2023 Local time: 07:31

Wapalestina wajitokeza Ramallah kuomboleza kifo cha hayati Shireen


Waombolezaji wakiwa pembeni ya mwili wa marehemu Shireen Abu Akleh, mwandishi wa habari wa Al Jazeera ambaye inadaiwa aliuawa katika mashambulizi ya bunduki wakati Israeli ilipovamia eneo hilo la Wapalestina.huko Jenin May 11, 2022. REUTERS/Mohamad Torokman

Mwandishi huyo aliuliwa alipokuwa anaripoti juu ya uvamizi wa jeshi la Israel kwenye kambi ya Wapaletina mjini Jenin huko Ukingo wa Magharibi. Serikali ya Israel inatoa wito wa kufanyika uchunguzi kutokana na mauaji ya mwandishi huyo.

Shireen Abu Aqleh, aliyekuwa na umri wa miaka 51 ni Marekani mwenye asili ya Kipalestina na mwandishi habari mashuhuri wa kituo cha televisheni chenye makazi yake Qatar.

Alikuwa mjini Jenin, Ukingo wa Magharibi akiwa amevaa koti la kujikinga na risasi lililokua limeandikwa Press, akiripoti juu ya kuongezeka kwa uvamizi wa jeshi la Israel kwenye kambi kuu ya mji huo kutokana na kuwepo na mashambulio katika mitaa ya Waarabu nchini Israel.

Al-Jazeera na mwandishi mwenzake aliyejeruhiwa Ali Samoudi wanawatuhumu wanajeshi wa Israel kwa mauaji yake lakini viongozi wa Israel wanasema huenda aliuliwa na risasi kutoka kwa Wapelestina.

Waziri Mkuu wa Israel Naftali Bennet katika taarifa anasema huenda aliuliwa kutokana na mshambulizi wa Wapalestina.

Waziri Mkuu wa Israeli Naftali Bennett
Waziri Mkuu wa Israeli Naftali Bennett

Waziri mkuu alieleza: Inasikitisha, mwandishi Habari wa Al Jazeera Shireen Abu Akleh aliuliwa wakati wamashambuklizi ya bunduki. Utawala wa Palestina umeilaumu haraka Israel kwa kifo chake, na rais wa utawala huo ametoa tuhumu zisizo za msingi dhidi ya Israel kabla ya uchunguzi kufanyika. Kulingana na Habari za awali tulizo nazo kuna uwezekano mkubwa mwandishi wa habari alipigwa na risasi kutoka kwa Wapalestina. Hata hivyo, ili kujua ukweli tuna hitaji uchunguzi wa kina na Wapalestina hivi sasa wanazuia jambo hilo.

Na Waziri wa Mambo ya Nje wa Israel Yair Lapid kupitia msemaji wake Lior Haiat anasema wameiomba serikali ya Palestina kushiriki kwenye uchunguzi.

Waziri wa Mambo ya Nje Yair Lapid
Waziri wa Mambo ya Nje Yair Lapid

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje anaeleza: "Tumesikitishwa na kifo cha mwandishi muandamizi wa Al Jazeera Shireen Abu Akleh wakati wa mapigano makali ya bunduki wakati wa operesheni ya kupambana na ugaidi mjini Jenin. Uhuru wa vyombo vya Habari ni haki msingi kwa Israel na kwa nchi zote za kidemokrasia, na hivyo ni lazima waandishi wa habari walindwe. Kuna ishara kwamba Bi Abu Akleh aliuliwa na risasi kutoka gaidi wa kipalestina, Israel itafanya uchunguzi wa kina. Tunatoa wito kwa Utawala wa palestina kushiriki kwenye uchunguzi ili kupata ukweli wa mambo."

Hata hivyo mwandishi habari wa kituo cha habari cha Altra Palestina aliyeshuhudia mashambulio hayo anasema risasi zilitoka upande wa wanajeshi wa Israel.

Mwandishi Habari wa kituo cha Altra Palestine anaeleza: "Kwanza Ali samoudi alipigwa kwa risasi na kuanguka, na aliweza kujiburura na kwenda sehemu nyingine. Halafu Sherine alianza kupiga kelele kwamba Ali kajeruhiwa. Mimi na yeye tulisimama karibu na ukuta na kuanza kusogea pole pole, mimi nikajikinga kwa kusimama nyuma ya mti na mara nikamuona mwenzangu ameanguka mara moja. Kila tulipojaribu kumkaribia wanajeshi wa Israel waliendelea kutufyetulia risasi, mashambulio hayakusita licha ya Ali na Shireen kujeruhiwa."

Kituo cha Al Jazeera kilisitisha matangazo yake na kueleza kifo cha Shireen na kutoa taarifa kwamba majeshi yanayokalia Palestina ikimaanisha majeshi ya Israel yamemua hadi mwandishi wa Al Jazeer huko Pelestina. Na kimetoa wito kwa jumuia ya kimataifa kuwawajibisha wanajeshi wa Israel kwa kulenga kwa maksudi na kumua mwandishi wake. Mbunge wa kiarabu nchini Israel Ahmed Tibi anailaumu pia serikali ya Israel.

Ahmed Tibi, Mbunge Muarabu wa Israel anaeleza: Serikali ya Israel inayongozwa na Naftali Bennett inawajibika kabisa na uhalifu huu. Wanalazimika kuchukuliwa hatua na jumuia ya kimataifa.

Wizara ya afya ya Palestina inasema kwamba Shireen alipigwa risasi ya kichwa. Waziri wa Paletina wa masuala ya Jerusalem Fadi al-Hadmi anasema haya ni mauaji ya kusikitisha.

Waziri wa Palestina wa masuala ya Jerusalem anaeleza: "Kwa kiwango cha ubinadamu tumempoteza Rafiki yetu Shireen, mwandishi Habari kutoka Jerusalem aliyewatetea Wapalestina na kila nyumba mjini Jerusalem kwa muda mrefu. Kwa upande wa Kisiasa ni ukatili na ubaguzi. Ina onyesha bayana unafiki wa kimataifa wakati Mpalesina anauliwa bila ya sababu hakuna anaelalamika. Hii si Ukraine hii ni Jenin. Tunasubiri kuona Jumuia ya kimataifa ikilaani kitendo hiki.

Jeshi la Israel kwenye taarifa yake inasema wanajeshi wake wanajibu mashambulio dhidi yao huko Jenin.

Msemaji wa ubalozi wa Marekani mjini Jerusalem ametoa taarifa ikisema kwamba Abu Akleh aliripoti juu ya masuala muhimu ya Mashariki ya Kati na Kimataifa kwa zaidi ya miongo miwili na alikuwa anaheshimiwa sana na Wapalestina wengi na watu wengine kote duniani.

Familia na marafiki wamekusanyika nyumbani kwake kuomboleza kifo chake. Na mwili wake umeswaliwa na kuzikwa tayari leo baada ya kumalizika kufanyiwa uchunguzi.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG