Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Oktoba 12, 2024 Local time: 21:52

Mpalestina apigwa risasi na wanajeshi wa Israel


Mwaandamanaji wa Palestina akirushia mawe maafisa wa uslama wa Israel katika ukanda wa magharibi APRIL 15 2022
PICHA: AFP
Mwaandamanaji wa Palestina akirushia mawe maafisa wa uslama wa Israel katika ukanda wa magharibi APRIL 15 2022 PICHA: AFP

Wanajeshi wa Israel wamempiga risasi na kumuua mwanamme mpalestina mwenye umri wa miaka 20 katika shambulizi lililotokea kwenye kambi ya wakimbizi, ukanda wa magharibi.

wizara ya afya ya Palestina imesema kwamba mwanamme huyo kwa jina Ahmad Oweidat, amepigwa risasi kichwani.

Jeshi limethibitisha kwamba lilitekeleza msako usiku wa kuamkia leo, katika kambi ya wakimbizi ya Aqbat Jabr, kusini mwa mji wa Jericho.

Limesema kwamba wanajeshi walianza mashambulizi ya risasi baada ya wapalestina kadhaa kuanza kuwarishia mawe, na mabomu ya moto.

Katika taarifa nyingine, jeshi la Israel limesema kwamba wapalestina 11, wanaodaiwa kuwa wapiganaji, wamekamatwa katika ukanda wa magharibi.

Mashambulizi hayo ya risasi yametokea siku chache baada ya kuongezeka kwa mvutano kati ya Israel na Palestina kufuatia mshambulizi makali ndani ya Israel, yaliyosababisha vifo vya watu kadhaa.

XS
SM
MD
LG