Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 08, 2023 Local time: 04:52

Wanawake wawili wa Kipalestina wauawa na wanajeshi wa Israel.


Wanajeshi wa kikosi cha usalama cha Israel wakipiga doria kwenye eneo kulikotokea mapambano kati ya maafisa wa usalama wa Israel na Wapalestina kwenye lango la Damascus katika mji wa zamani wa Jerusalem. April 4, 2022. Picha ya Reuters.
Wanajeshi wa kikosi cha usalama cha Israel wakipiga doria kwenye eneo kulikotokea mapambano kati ya maafisa wa usalama wa Israel na Wapalestina kwenye lango la Damascus katika mji wa zamani wa Jerusalem. April 4, 2022. Picha ya Reuters.

Wanajeshi wa Israel Jumapili wameua wanawake wawili wa Kipalestina baada ya mmoja kuwakimbilia wanajeshi na mwingine kumchoma kisu mwanajeshi katika matukio tofauti katika Ukingo wa magharibi unaokaliwa kimabavu, maafisa wa usalama wa Israel wamesema.

Umwagaji damu huo unafuatia msururu wa mashambulizi mabaya ya Waarabu nchini Israel.

Kumekuwa pia operesheni za uvamizi za Israel ndani na kuzunguka mji wa Jenin huko Ukingo wa magharibi, ngome ya wanamgambo, dhidi ya kile waziri mkuu Naftali Bennett imeiita ni “wimbi jipya la ugaidi.”

Hakuna silaha iliyopatikana kwenye mwili wa mwanamke aliyepigwa risasi huko Bethlehem baada ya kupuuza wito wa wanajeshi na onyo la kufyatua risasi kuacha kuwakaribia wanajeshi, jeshi la Israel limesema, na kuongeza kuwa limeanzisha uchunguzi kuhusu tukio hilo.

Katika tukio la pili, mwanamke aliyejihami kwa kisu aliuawa kwa kupigwa risasi baada ya kumjeruhi kidogo afisa wa polisi wa mpakani huko Hebron, nje ya eneo la makaburi, ambalo Waislamu wanaliita Mskiti wa nabi Ibrahim, maafisa wa usalama wa Israel wamesema.

Wizara ya afya ya Palestina imethibitisha vifo hivyo viwili.

XS
SM
MD
LG