Katika taarifa iliyochapishwa kwenye mtandao wa Facebook, kikundi kiitwacho Living Forces kilisema vijana wanne wenye umri kati ya miaka 15-18 walifariki siku ya Jumatatu na Jumanne. Awali walitaja idadi ya watu wawili.
Vifo hivyo vimefanya jumla ya vifo vilivyosababishwa na vikosi vya usalama tangu mwezi Juni mwaka 2022 kufikia 30, ilisema taarifa hiyo.
Taifa hilo maskini la Afrika Magharibi ambalo limekuwa likitawaliwa na jeshi tangu Septemba 5, 2021, baada ya wanajeshi kumuondoa madarakani rais mteule wa nchi hiyo Alpha Conde.
Mwezi June mwaka mmoja baadaye, utawala wa kijeshi uliimarisha msimamo wake huku upinzani ukipiga kelele juu ya haki na demokrasia.
Tangu wakati huo, watu 108 wamejeruhiwa na zaidi ya mamia kukamatwa na kuwekwa kizuizini kiholela, kulingana na Living Forces.
Wakijiandaa kwa maadhimisho hayo, mamlaka ilisisitiza amri iliyokuwa imeiweka Mei 2022, iliyozuia "harakati za uungaji mkono na maandamano kwenye barabara za umma ... ili kulinda amani."
Hakuna sherehe zilizofanyika kwa maadhimisho hayo, lakini viongozi wa kijeshi walijitokeza kwenye vyombo vya habari vya ndani wakitetea rekodi yao, ikiwa ni pamoja na kuwekeza katika mahospitali na kuunda mahakama maalumu ili kushughulikia uhalifu wa kifedha.
Kutokana na shinikizo la kimataifa, utawala wa kijeshi umeahidi kurejesha utawala wa kiraia ifikapo mwisho wa 2024, ikidaiwa kupewa muda wa kutosha ili kufanya mageuzi ya kitaasisi.
Lakini Living Forces inasema hakuna maendeleo kwa rasimu ya katiba, kanuni za uchaguzi au chombo kwa ajili ya kusimamia uchaguzi, ikiwa ni miongoni mwa hatua muhimu zinazohitajika ili kurejea katika utawala wa kiraia.
Chanzo cha habari ni Shirika la habari AFP
Forum