Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Machi 18, 2025 Local time: 04:03

Utawala wa kijeshi Guinea wawaonya watakaoandamana


Kanali Mamady Doumbouya (katikati) akiwa na na timu yake Ikulu Septemba 14, 2021. Picha na JOHN WESSELS / AFP.
Kanali Mamady Doumbouya (katikati) akiwa na na timu yake Ikulu Septemba 14, 2021. Picha na JOHN WESSELS / AFP.

Utawala wa kijeshi katika taifa la Afrika magharibi la Guinea wameonya dhidi ya wale ambao watajiunga katika maandamano siku ya Jumanne, wakati utawala huo ukiadhimisha miaka miwili tangu unyakue mamlaka.

Marufuku hiyo inahusu maandamano yaliyopangwa na upinzani unaotaka kurejeshwa haraka kwa utawala wa kiraia. Jumatatu jioni mamlaka ilitoa taarifa ikirejea amri iliyoitoa mwezi Mei mwaka jana ambayo iliharamisha "harakati za uungaji mkono na maandamano" kwenye barabara za umma.

Utawala huo uliwaonya watu watakao kiuka amri hiyo, ambayo walisema iliwekwa ili "kulinda amani."

Nchi hiyo ambayo haina utulivu, imekuwa ikitawaliwa na jeshi tangu Septemba 5, 2021, baada ya kupindiliwa rais Alpha Conde, kiongozi wa kwanza wa nchi hiyo aliyechaguliwa na wananchi.

Pamoja na kupiga marufuku maandamano yote, utawala wa kijeshi umewakamata viongozi kadhaa wa upinzani na baadhi yao kuwafungulia mashtaka.

Mkusanyiko wa vyama na mashirika yanayoitwa Living Forces yaliitisha maandamano ya "amani" wakati wa utawala huo wa kijeshi ukiadhimisha miaka miwili tangu ulipofanya mapinduzi.

Katika taarifa yake, Living Forces inaishitumu serikali ya kijeshi kutofanya lolote katika kurudisha mamlaka mikononi mwa raia.

Miongoni mwa mambo mengine, taarifa hiyo imeangazia ukosefu wa maendeleo kwa rasimu ya katiba, kanuni za uchaguzi au chombo cha kusimamia uchaguzi.

Chanzo cha habari ni Shirika la habari AFP

Forum

XS
SM
MD
LG