Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Septemba 26, 2023 Local time: 05:41

Wachambuzi wadai waliompindua Bongo Gabon walijipanga vizuri


Rais wa Gabon Omar Bongo Ondimba (kushoto) akizungumza na Paul Biya (kulia) huku Jenerali Brice Oligui Nguema akiwa katikati huko Libreville, Agosti 17, 2007. Picha na WILS YANICK MANIENGUI / AFP.

Wanajeshi waliomuondoa madarakani rais wa Gabon wanaonekana walijipanga vizuri na kutumia malalamiko ya wananchi dhidi ya serikali kuwa kisingizio cha kunyakua mamlaka, wachambuzi walisema.

Jumatano wanajeshi walimtimua Rais Ali Bongo Ondimba, ambaye familia yake ilitawala katika nchi hiyo yenye utajiri wa mafuta , huko Afrika ya Kati kwa zaidi ya miongo mitano.

Viongozi wa mapinduzi walimshutumu Bongo kwa utawala usiokuwa na uwajibikaji, hivyo kuhatarisha nchi hiyo kuingia katika machafuko na kusema imemuweka rais huyo katika kizuizi cha nyumbani na pia kuwaweka vizuizini wajumbe kadhaa wa Baraza la Mawaziri.

Wakati huo huo, Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika lilikutana Alhamisi na kutangaza kuisimamisha haraka Gabon kutoka "shughuli zote za AU, vyombo vyake na taasisi" hadi itakapo rejesha utaratibu wa kikatiba katika nchi hiyo.

Siku ya Ijumaa shirika la habari la Reuters limeripoti kuwa kundi kuu la upinzani la Alternance 2023, limeitaka jumuiya ya kimataifa kuushawishi utawala wa kijeshi kurudisha mamlaka kwa raia.

Mkuu wa kikosi maalum cha ulinzi huko Gabon, Jenerali Brice Clotaire Oligui Nguema, alitangazwa kwenye Televisheni ya taifa kuwa kiongozi mpya wa taifa hilo, saa chache baada ya Bongo kutangazwa kuwa mshindi wa uchaguzi wa rais uliofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita ambao waangalizi walisema uligubikwa na kasoro na ukosefu wa uwazi.

Ingawa kulikuwa na malalamiko halali kuhusu kura na utawala wa Bongo, kuondolewa kwake madarakani ni kisingizio tu cha utawala wa kijeshi kutwaa madaraka, wataalam wa Gabon wanasema.

Katika tangazo lililorushwa kwenye televisheniya serikali siku ya Alhamisi, msemaji wa utawala wa kijeshi alisema Oligui ataapishwa Jumatatu kwenye mahakama ya kikatiba. Iliwahimiza watu kurudi kazini na kusema itarejesha usafiri wa ndege wa ndani.

Jenerali Brice Oligui Nguema (Kulia) alipopewa nishani na Waziri Mkuu wa Gabon Alain Claude Bilie Bie Nze (kushoto). Picha na AFP.
Jenerali Brice Oligui Nguema (Kulia) alipopewa nishani na Waziri Mkuu wa Gabon Alain Claude Bilie Bie Nze (kushoto). Picha na AFP.

Alhamisi pia, upinzani wa kisiasa wa Gabon ulitoa wito wa kurudiwa kwa uchaguzi "chini ya usimamizi" wa majeshi," ili kuruhusu mgombea mkuu wa upinzani, Albert Ondo Ossa, kushika wadhifa wa urais, alisema meneja wake wa kampeni Mike Jocktane.

Tofauti na Niger na nchi jirani za Burkina Faso na Mali, ambazo zimeshuhudia mapindiuzi mawili tangu mwaka 202, ambazo zinakumbwa na ghasia za wenye msimamo mkali, Gabon kwa kiasi kikubwa ilikuwa thabiti.

Ufaransa mtawala wa zamani wa kikoloni ambayo ni mwanachama wa OPEC, lakini utajiri wake wa mafuta uko kwenye mikono ya watu wachache - takribani asilimia 40 ya Wagabon wenye umri kati ya miaka 15 hadi 24 hawana ajira, kulingana na Banki ya Dunia mwaka 2020.

Mapato yake ya mauzo ya nje ya mafuta yalikuwa dola bilioni sita mwaka 2022, kulingana na Utawala wa Habari wa Nishati wa Marekani.

Baadhi ya taarifa hii inatoka shirika la habari la Reuters

Forum

XS
SM
MD
LG