Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Septemba 18, 2024 Local time: 10:05

Niger imefungua tena njia zake za angani


Niger imefungua tena njia zake za angani baada ya mapinduzi nchini humo hivi karibuni. Aug. 1, 2023
Niger imefungua tena njia zake za angani baada ya mapinduzi nchini humo hivi karibuni. Aug. 1, 2023

Uwanja wa ndege wa Jamhuri ya Niger uko wazi kwa safari zote za ndege za kitaifa na kimataifa, shirika hilo limemnukuu msemaji wa wizara ya uchukuzi akisema, akiongeza kuwa huduma kwa njia za ardhini pia zimeanza tena

Niger Jumatatu ilifungua tena anga yake karibu mwezi mmoja baada ya kuweka marufuku kufuatia mapinduzi ya kijeshi mwezi Julai, shirika la habari la Niger ANP limesema.

Baada ya kuchukua madaraka Julai 26 viongozi wa mapinduzi walifunga anga ya nchi hiyo kabla ya kuifungua tena Agosti 2, hatua ambayo ilibadilishwa Agosti 6 baada ya nchi za kikanda kutishia kuingilia kijeshi kurejesha utawala wa kiraia.

Uwanja wa ndege wa Jamhuri ya Niger uko wazi kwa safari zote za ndege za kitaifa na kimataifa, shirika hilo limemnukuu msemaji wa wizara ya uchukuzi akisema, akiongeza kuwa huduma kwa njia za ardhini pia zimeanza tena. Imeongeza kuwa anga ya Niger bado imefungwa kwa ndege zote za kijeshi na zingine zinazohitaji idhini ya awali kutoka kwa mamlaka husika.

Jumuiya ya Kiuchumi ya nchi za Afrika Magharibi imeiwekea vikwazo Niger baada ya kuondolewa madarakani kwa rais Mohamed Bazoum na jumuiya hiyo kutishia kuingilia kijeshi kama njia ya mwisho iwapo mazungumzo yatashindwa kurejesha utawala wa kiraia. Agosti 2, Niger ilifungua tena mipaka ya ardhini na angani kwa nchi tano jirani, ambazo ni Algeria, Burkina Faso, Libya, Mali na Chad.

Forum

XS
SM
MD
LG