Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 08:57

Wananchi wajitokeza kupiga kura kumchagua rais Iran


Ebrahim Raisi, mmoja wa wagombea urais akinyanyua mikono yake wakati alipomaliza kupiga kura huko Tehran, Iran, Ijumaa, Juni 18, 2021.
Ebrahim Raisi, mmoja wa wagombea urais akinyanyua mikono yake wakati alipomaliza kupiga kura huko Tehran, Iran, Ijumaa, Juni 18, 2021.

Wananchi wa Iran wanapiga kura Ijumaa kumchagua rais mpya. 

Katika uchaguzi huu wa urais ambao unaelezwa kwamba mshindi wake huenda akawa ni yule anayeungwa mkono na Kiongozi Mkuu wa nchi hiyo, Ayatolla Ali Khamenei.

Uungaji mkono huu ni jambo ambalo limepelekea baadhi ya watu kupungukiwa na imani, na kusababisha kutolewa kwa wito wa kususia zoezi hilo.

Utafiti wa maoni pamoja na wachambuzi wanamtaja jaji mkuu wa nchi hiyo Ebrahim Raisi ambaye ana msimamo mkali kama aliye katika nafasi bora ya kushinda uchaguzi huo, ambao umevutia wagombea wanne pekee.

Kuna zaidi ya wapiga kura milioni 59 nchini Iran, taifa ambalo lina watu zaidi ya milioni 80. Lakini shirika la wanafunzi la utafiti lenye uhusiano na serikali ya nchi hiyo, linakadiria kwamba idadi ya waliojitokeza ni 42% tu, ambayo itakuwa chini zaidi, tangu mapinduzi ya Kiislamu ya mwaka 1979, yaliyofanyika nchini humo.

Kwa mujibu wa katiba ya Iran, rais wa sasa Hassan Rouhani, hawezi kuwania tena kwa sababu amekamilisha mihula yake miwili.

Chanzo cha Habari : VOA News

XS
SM
MD
LG