Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Septemba 15, 2024 Local time: 23:56

Moto unaendelea kuteketeza kiwanda cha kusafisha mafuta Iran


Moto ukiwaka katika kiwanda cha kusafisha mamuta katika mji mkuu wa Iran, Tehran. (Photo by Vahid AHMADI / TASNIM NEWS / AFP)
Moto ukiwaka katika kiwanda cha kusafisha mamuta katika mji mkuu wa Iran, Tehran. (Photo by Vahid AHMADI / TASNIM NEWS / AFP)

Moto mkubwa kwenye kiwanda cha kusafisha mafuta karibu na mji mkuu wa Iran, Tehran ulikuwa unawaka kwa siku ya pili  Alhamisi, wakati vikosi vya zimamoto vikiendelea kujitahidi kuuzima moto huo.

Moto ulianza katika kampuni inayomilikiwa na serikali ya Tondgooyan Petrochemical Co kusini mwa Tehran, Jumatano usiku ukipeleka moshi mzito angani katika mji huo mkuu.

Shirika la habari la Wizara ya mafuta, SHANA, limesema moto ulizuka kutokana na kuvuja kwa matanki mawili ya taka katika kituo hicho.

Awali, viongozi walisema moto huo uliathiri bomba la gesi ghafi kwenye kiwanda hicho cha kusafisha mafuta.

Waziri wa mafuta Bijan Zanganeh alitembelea eneo la ajali nyakati za usiku, huku akiwahakikishia wananchi kwamba moto huo hautoathiri uzalishaji mafuta.

Wananchi wa Iran wameonekana leo asubuhi majira ya huko, wamepanga foleni kwa ajili ya kununua mafuta.

XS
SM
MD
LG