Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 18:29

Mapigano kati ya serikali na waasi wa kihouthi yaua watu 70 Yemen


FILE PHOTO: Wafuasi wa Kihouthi wakiwa juu ya Lori baada ya kushiriki katika maziko ya wapiganaji wa Kihouthi waliouawa wakipambana na majeshi ya serikali katika jimbo lenye utajiri wa petroli, Marib, Sanaa, Yemen.
FILE PHOTO: Wafuasi wa Kihouthi wakiwa juu ya Lori baada ya kushiriki katika maziko ya wapiganaji wa Kihouthi waliouawa wakipambana na majeshi ya serikali katika jimbo lenye utajiri wa petroli, Marib, Sanaa, Yemen.

Mapigano kati ya vikosi vya serikali inayotambuliwa kimataifa ya Yemen na waasi wa Kihouthi yaliendelea katika majimbo ya Marib na Taiz, na kusababisha vifo vya wapiganaji wasiopungua 70 pande zote mbili.

Katika mapigano hayo watu wengine wapatao 85 wamejeruhiwa, maafisa wa jeshi na upande wa waasi walieleza.

Waasi wanaoungwa mkono na Iran, mwezi Februari 2021, walifanya mashambulio mapya, katika jimbo lenye utajiri wa mafuta la Marib, ngome inayoshikiliwa na serikali, na ambayo inamvutano na Wahouthi.

Shambulio la Marib lilichochea vurugu katika maeneo mengine, pamoja na mkoa wa Tazi unaoshikiliwa na serikali, ambao umezingirwa na Wahouthi.

Maafisa hao walisema wapiganaji wasiopungua 42 waliuawa huko Marib na 28 huko Taiz.

Wengi wa waliokufa walikuwa ni waasi, kwa mujibu wa afisa wa jeshi na upande wa wasi, waliozungumza kwa sharti la kutotajwa, kwa kuwa hawakuruhusiwa kuzungumza na vyombo vya habari.

XS
SM
MD
LG