Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 09, 2022 Local time: 02:29

UN kuchangisha dola bilioni 3.85 kukabiliana na njaa Yemen


Wanawake wakisubiri msaada wa chakula katika kituo cha kutibu utapiamlo huko Hospitali ya al-Sabeen, Sanaa, Yemen February 24, 2021. REUTERS/Khaled Abdullah

Umoja wa Mataifa unatarajia kuchangisha karibu dola bilioni 3.85 Jumatatu katika juhudi za kuzuia janga kubwa la njaa linalo wakabili wananchi wa Yemen.

Umoja huo unasema maisha katika taifa hilo linalokumbwa na vita ni mabaya ziadi na kwamba watoto wanakufa.

Zaidi ya mataifa 100 na wafadhli wanashiriki kwenye mkutano huo ambao kwa sehemu kubwa unafanyika kupitia mtandao na kufadhiliwa na Sweden na Uswizi.

Mkutanio huo unafanyika wakati Wahouthi wa Yemen wakizidisha mapigano huku wakijaribu kuchukua udhibiti wa jimbo la mwisho la kaskazni linaloshikiliwa na serikali la Mirbid.

Mwaka wa 2019 UN na washirika wake walipokea dola bilioni 1.9 kiasi cha nusu ya fedha walichohitaji, lakini msaada huo ukapunguka sana mwaka 2020 kutokana na janga la Corona pamoja na kuporomoka kwa uchumi duniani.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG