Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 25, 2024 Local time: 17:29

Biden aanza msukumo wa kidiplomasia kufufua mkataba wa nyuklia wa Iran


Rais Joe Biden akizungumza katika mkutano wa Usalama wa Munich kwa njia ya mtandao.
Rais Joe Biden akizungumza katika mkutano wa Usalama wa Munich kwa njia ya mtandao.

Rais wa Marekani Joe Biden ameanza msukumo wa kidiplomasia kufufua mkataba wa nyuklia wa mwaka 2015 kati ya Iran na mataifa yenye nguvu duniani.

Wanaounga mkono makubaliano hayo wanasema atahitaji juhudi za muda mrefu kufanikisha, wakati wapinzani wanasema ajikite badala ya kuishinikiza Tehran kuingia makubaliano mapya na mazito zaidi.

Mkataba wa 2015, JCPOA, ulifikiwa kati ya Iran na wanachama watano wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ikiwemo Ujerumani, wanaojulikana kama “P5+1.”

FILE - Washiriki wa mkutano wa JCPOA.
FILE - Washiriki wa mkutano wa JCPOA.

Mkataba huu unaitaka Iran kupunguza harakati za nyuklia kwa kipindi kati ya miaka minane hadi 15 ili kuachana na mpango wa utengenezaji wa silaha kwa mabadilishano ya kupatiwa ahueni ya vikwazo vya vikwazo vya kimataifa.

Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump alijiondoa kutoka katika mkataba huo mwaka 2018 akisema ulikuwa hauna nguvu za kutosha kuidhibiti Iran, na kupelekea Iran kukiuka makubaliano ya nyuklia tangu 2019.

FILE PHOTO: Rais Donald Trump
FILE PHOTO: Rais Donald Trump

“Tuko tayari kurejea tena katika mashauriano na P5 + 1 juu ya programu ya nyuklia ya Iran,” Biden amesema Ijumaa akiwa White House, katika hotuba aliyoitoa katika mkutano wa kila mwaka wa sera ya Usalama wa Munich uliofanyika kwa njia ya mtandao.

Biden, ambaye ameahidi kurejea kwenye JCPOA iwapo kwanza Iran itatekeleza tena mkataba huo kikamilifu, itatoa jawabu chanya kwa pendekezo lililotolewa na Umoja wa Ulaya Alhamisi likizitaka nchi sita zenye nguvu duniani na Iran kuhudhuria mkutano usio rasmi kujadili vipi wataufufua mkataba huo.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje amesema Marekani itakubali mwaliko huo, ambao bado haujatolewa hadharani.

Utawala wa Biden ulitoa ishara nzuri kwa Iran, ukiondoa ombi la Trump katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa akisukuma “haraka” vikwazo dhidi ya Iran, ombi ambalo wanachama wengine wa baraza hilo wengine walilikataa, na kuondoa baadhi ya vikwazo vya kusafiri vilivyowekwa kwa wanadiplomasia wa Iran wanaofanya kazi Umoja wa Mataifa, New York.

XS
SM
MD
LG