Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 09:03

Marekani na Iran wafanya mazungumzo yasiyo ya moja kwa moja juu ya wafungwa


Mazungumzo yasiyo ya moja kwa moja ya Marekani na Iran huko Vienna
Mazungumzo yasiyo ya moja kwa moja ya Marekani na Iran huko Vienna

Mwezi uliopita msemaji wa serikali ya Iran, Ali Rabiei, alitoa wito kwa Marekani kuwaachia wafungwa wote wa Iran ambao anasema wamewekwa kizuizini kimakosa kwa kukiuka vikwazo vya Marekani dhidi ya Iran

Wakati Marekani na Iran zinafanya mazungumzo yasiyo ya moja kwa moja kuhusu kushiriki katika mabadilishano nadra ya wafungwa, waangalizi wanaelezea tathmini mpya kuhusu idadi ya wairan wasiojulikana waliopo kwenye kizuizi cha Marekani au mashtaka ambayo yanaweza kujumuishwa katika ubadilishanaji huo wa wafungwa.

Maafisa wa Marekani na Iran wanasema pande hizo mbili zimekuwa zikijadiliana suala la wafungwa kupitia wapatanishi katika wiki za hivi karibuni kipindi ambacho maadui wa muda mrefu pia wamefanya mazungumzo yasiyo ya moja kwa moja huko Vienna yenye lengo la kufufua makubaliano ya nyuklia ya mwaka 2015 kati ya Iran na mataifa yenye nguvu duniani.

Mwezi uliopita msemaji wa serikali ya Iran, Ali Rabiei, alitoa wito kwa Marekani kuwaachia wafungwa wote wa Iran ambao anasema wamewekwa kizuizini kimakosa kwa kukiuka vikwazo vya Marekani dhidi ya Iran.

Rabiei hakutaja majina ya wafungwa au idadi ya wafungwa hao isipokuwa alielezea kwamba idadi ni kubwa kuliko wamarekani wanne ambao Iran inawashikilia huko.

XS
SM
MD
LG