Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Machi 20, 2023 Local time: 19:50

Wananchi wa DRC wanamatumaini ziara ya Papa Francis itahamasisha uchaguzi huru na wa haki


Papa Francis

Wakatoliki huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, ambako Kanisa Katoliki kwa muda mrefu limekuwa na ushawishi mkubwa, wana matumaini Papa Francis wakati wa ziara yake wiki ijayo ataomba uchaguzi uwe huru na wa haki.

Kampeni tayari zimeanza kwa ajili ya uchaguzi wa urais mwezi Desemba, kipindi ambacho mara nyingi kimejaa maandamano na vurugu na shutuma za ubadhirifu baada ya miongo kadhaa ya utawala wa kimabavu.

Mara nyingi kanisa limekuwa likikabiliana na serikali ya taifa hilo la Afrika ya Kati, lenye utajiri wa madini lakini maskini ambalo linakadiriwa asilimia 40 ya watu wake milioni 100 ni Wakatoliki.

Tangu Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ipate uhuru wake kutoka Ubelgiji mwaka 1960, Ukatoliki umedumisha "kukua kwa maadili", alisema mwanasayansi wa siasa Christian Moleka.

"Linabakia kuwa njia ya kukimbilia kwa masuala makubwa yenye maslahi ya kitaifa," aliiambia AFP.

Katika miaka ya karibuni Kanisa limeweka wasimamizi wa uchaguzi na kutumia ushawishi wake kuwashinikiza viongozi waliochaguliwa kuheshimu ukomo wa mihula ya kikatiba.

Kura ya urais, wakati Felix Tshisekedi atasimama kuwania muhula wa pili baada ya uchaguzi wake kuzua mzozo mwaka 2018 , huenda ukazua mjadala wakati wa ziara ya siku nne ya Papa Francis.


Chanzo cha habari hii ni gazeti la "The East African" linalochapishwa nchini Kenya.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG