Baba Mtakatifu Francis aliwaongoza maelfu ya waombolezaji waliohudhuria ibada maalum ya mazishi ya aliyekuwa kiongozi wa kanisa Katoriki, papa Benedict, iliyofanyika katika eneo la St. Peter. Papa Francis amemfananisha kiongozi huyo na Yesu. Sauti za kengele zilisikika, watu kumi na mbili walibeba jeneza lililotengenezwa kwa mbao, likiwa na mwili wa papa Benedict kabla ya mazishi yatakayofanyika katika kanisa kubwa kuliko yote huko Christendom. Makofi yalisikika pande zote, zilizojaa umati mkubwa wa watu, hii ni dalili ya heshima kubwa kwa papa Benedict. Shujaa wa waumini wa kanisa katoliki aliyeishangaza dunia katika uongozi wake wa karibu muongo mmoja pale alipotangaza kujiuzuu upapa. Akiongoza ibada hiyo ya mazishi , Francis alinukuu maandishi ya biblia na maandiko ya kanisa ambayo yalionyesha kumlinganisha Benedict na Yesu, yakiwemo maneno yake ya mwisho kabla ya kifo chake msalabani: “baba, mikononi mwako, naiweka roho yangu” Papa Francis pia alitumia maandiko mengine ya biblia alimfananisha Benedict na Yesu yakiwemo “upendo maana yake kuwa yuko tayari kuteseka” na waumini waliitikia “tunamuweka nduyu yetu mikononi mwako bwana”
Hayati Benedict azikwa, Papa Francis amfananisha na Yesu
Matukio
-
Februari 04, 2023
Wananchi wa Peru washinikiza kufanyika uchaguzi, waandamana
-
Februari 04, 2023
Mkazi wa Haiti anayejulikana kimataifa, akanusha kujihusisha na uhalifu
-
Februari 04, 2023
VOA Mitaani: Uamuzi wa Mahakama Kuu Kenya waibua hisia mseto
-
Februari 03, 2023
Seneta Michael Bennette ataka programu ya TikTok kuondolewa
-
Februari 03, 2023
Nairobi: Mkazi wa Dandora aeleza uchafuzi wa mazingira ulivyauathiri mto