Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Mei 25, 2024 Local time: 20:21

Afrika: Maandalizi ya Papa Francis kuzuru DRC na Sudan Kusini yakamilika


Papa François alipokutana na Rais Félix Tshisekedi mjini Vatican, Januari 17, 2020.
Papa François alipokutana na Rais Félix Tshisekedi mjini Vatican, Januari 17, 2020.

Papa Francis amejiandaa kwenda  Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Sudan Kusini mwishoni mwa mwezi huu – ziara ambayo hapo awali alilazimika kuiakhirisha kwa sababu za kiafya.

Papa Francis anatarajiwa kuitembelea DRC kuanzia Januari 31 hadi Februari 3, na baadaye atakwenda Sudan Kusini kwa ziara ya siku mbili kabla kurejea Vatican. Wakati ofisi ya Holy See lilipotangaza ziara hiyo ambayo iliakhirishwa kutokana na matatizo ya magoti wakati wa majira ya joto mwaka jana, ilisema kuwa Askofu wa Canterbury na Mratibu wa Baraza Kuu la Kanisa la Scotland watasafiri na papa.

Papa ataanzia safari yake Kinshasa, ambako atakutana na viongozi wa nchi hiyo, waathirika wa vita vya mashariki mwa nchi hiyo, na pia atakutana na wawakilishi wa taasisi za hisani. Baadaye atasafiri kwa ndege kuelekea Juba, mji mkuu wa Sudan Kusini.

Kinshasa, mji mkubwa na wenye umaskini una wakazi zaidi ya millioni 10, unafanyiwa maandalizi kwa ajili ya ziara ya papa. Mwakilishi wa Vatican nchini DRC Ettore Balestrero, amesema juhudi kubwa zinafanywa kuhakikisha usalama na utulivu wa umma wakati papa atakapokuwa nchini humo. Ni mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 37 tangu kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani alipoitembeleea nchi hiyo, na Balestrero alisema kuwa kwa walio wengi ujio wa papa Francis ni “ndoto iliyotimia.”

Katika mahojiano na Vatican News, askofu amesema, lengo kubwa la ziara ya papa nchini DRC ni “ kuamsha imani kwa wale ambao hawana na kuleta furaha zaidi kwa wale waliyo nayo” na kuongeza kuwa “nchi nzima inatarajia kupokea maneno ya faraja na ya kuponya vidonda ambavyo bado ni vibichi, hususan eneo la mashariki”

Kanisa la CEPAC lililoshambuliwa na wanaoshukiwa kuwa magaidi, nchini DRC.
Kanisa la CEPAC lililoshambuliwa na wanaoshukiwa kuwa magaidi, nchini DRC.

Jumanne Papa Francis alituma salamu za rambirambi kwa waathirika wa bomu katika kanisa la Pentekoste huko Kasindi, katika jimbo la Kivu Kaskazini, mashariki mwa Congo. Wanamgambo wa Kiislam wamedai kuhusika na shambulio hilo ambalo limeuwa watu wapatao 14 na kujeruhi watu zaidi ya 60. Awali papa alipanga kuutembelea mji wa Goma uliopo Kivu Kaskazini lakini safari hiyo iliahirishwa kutokana na ghasia zinazoendelea kuathiri maeneo ya jimbo.

Akiwa Sudani Kusini, papa Francis atakutana na watu waliokosheshwa makazi ndani ya nchi na kushiriki misa inayojumusha madhehebu mbalimbali ya Kikistristo itakayofanyika kwenye makaburi ya John Garang mjini Juba, ambako pia atashiriki misa ya Jumapili kabla ya kurejea Vatican.

XS
SM
MD
LG