Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Juni 20, 2024 Local time: 21:15

Papa mstaafu Benedict XVI afariki dunia


Papa Benedict
Papa Benedict

Papa Mstaafu Benedict XVI, ambaye aliongoza Kanisa Katoliki kwa takriban miaka minane kabla ya kuwa Papa wa kwanza kujiuzulu katika miaka 600, alifariki Jumamosi akiwa na umri wa miaka 95.

Kifo cha Benedict kilifuatia ombi la Papa Francis la kumwombea mtangulizi wake, huku Vatican ikitangaza afya ya Papa huyo wa zamani ilikuwa ikidorora kutokana na umri mkubwa.

Vatican inasema mwili wa papa huyo wa zamani utalala katika Kanisa kuu la Mtakatifu Petro kuanzia Jumatatu. Papa Francis ataadhimisha Misa ya mazishi ya Benedict katika uwanja wa Mt. Petro alhamisi.

Alipotoa tangazo la mshtuko mwaka 2013 kwamba atajiuzulu, Benedict alisema hana tena nguvu za kimwili na kiakili za kuhudumu kama Papa.

Hakujitokeza hadharani mara chache sana alipostaafu, akitoa miaka ya mwisho ya maisha yake kwa sala na kutafakari alipokuwa akiishi katika nyumba ya watawa huko Vatikani.

Katika barua ya 2018 katika gazeti la Corriere della Sera la Italia, Benedict alielezea "kupungua taratibu kwa nguvu zangu za mwili," akisema alikuwa "katika safari ya ndani kuelekea nyumbani."

XS
SM
MD
LG