Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Mei 28, 2024 Local time: 05:15

Wanamgambo washambulia gereza Burkina Faso, wawaachilia wafungwa 60

Raia wa Burkina Faso.
Raia wa Burkina Faso.

Wanamgambo wamewaachilia takriban wafungwa 60 katika shambulizi kwenye gereza moja iliyoko kaskazini magharibi mwa Burkina Faso usiku wa kuamkia Jumapili, na kupora ofisi na kuchoma moto magari kabla ya kukimbia, wamesema hayo maafisa wawili wa usalama pamoja na chanzo cha mahakama.

Watu waliokuwa na silaha walivamia mji wa Nouna majira ya usiku wakiwa kwenye pikipiki na kubeba bunduki, maafisa wa usalama wameongeza kusema hayo.

Wanamgambo waliwatorosha takriban wafungwa 60. Burkina Faso inapambana na uasi wa kigaidi ambao umeenea katika nchi jirani ya MALI katika muongo uliopita.

katika siku zilizopita ghasia kama hizo zilionekana kama kawaida. Wengi wameuwawa katika eneo hilo, na mamilioni ya watu wamelazimika kuhama nyumba zao.

Hata hivyo hakuna aliyeuawa katika shambulizi la wiki hii kwenye gereza, na hakuna kundi lolote lililodai kuhusika na shambulizi.

Tukio hilo limetokea ndani ya saa kadhaa wakati wanamgambo wasiojulikana walipouwa watu 11 katika miji kaskazini mwa Dori na Gargadji hiyo ni kwa mujibu wa maafisa kutoka eneo la ndani.

Miongoni mwa waliokufa katika shambulizi hilo walikuwa raia wawili na wanamgambo tisa.

Hata hivyo jeshi la Burkina Faso lilitangaza Ijumaa kwamba wanajeshi wengine 11 pamoja na maafisa wa polisi NA wanamgambo wameuwawa katika mashambulizi tofauti wiki iliyopita .

XS
SM
MD
LG