Operesheni hiyo iliyopewa jina la Taanli 3 iliendeshwa kati ya tarehe 2 na 25 Aprili ilifanikishwa na ndege za upelelezi na kivita, wakuu wa majeshi ya nchi hizo mbili wamesema katika ripoti.
Wamesema operesheni hiyo “iliua takriban magaidi 100,” 40 walikamatwa, iliharibu ngome 40 za wanajihadi na kupokonya vifaa vyao.
Wameongeza kuwa wanajeshi wawili walifariki na wengine wawili kujeruhiwa, bila kutaja uraia wao.
Niger na Burkina Faso zimekuwa zikishambuliwa na uasi wa kijihadi ulioanzishwa kutoka nchi jirani ya Mali mwaka 2015.
Maelfu ya watu waliuawa na maelfu ya wengine walitoroka makazi yao kutokana na uasi huo.