Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Februari 01, 2023 Local time: 19:37

Mkuu wa UN anatoa wito kwa vikosi vya Mali, Burkina Faso na Guinea kurudisha utawala wa kiraia


Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akizungumza na waandishi wa habari mjini Dakar wakati wa ziara yake huko Senegal. May 1, 2022.

Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres alitoa wito Jumapili kwa vikosi vya kijeshi vya Burkina Faso, Guinea, na Mali kurudisha madaraka kwa raia haraka iwezekanavyo na kuukumbusha ulimwengu kutekeleza ahadi za dharura za hali ya hewa.

Akizungumza baada ya kukutana na Rais wa Senegal Macky Sall mjini Dakar alisema wamekubaliana juu ya haja ya kuendelea kuzungumza na mamlaka ya ukweli katika nchi zote tatu ili kurejesha haraka kwa utaratibu wa kikatiba.

Nchi zote tatu zinapambana na uasi wa wanajihadi katika eneo la Sahel hivi karibuni zimekumbwa na mapinduzi ya kijeshi. Mali ilishuhudia tukio hilo mwezi Agosti mwaka 2020 na Mei mwaka 2021. Guinea Septemba mwaka 2021 na Burkina Faso ilikuwa Januari mwaka 2022.

Sall ndie mwenyekiti wa sasa wa Jumuiya ya Nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS) ambayo imezisimamisha uanachama nchi zote tatu.

ECOWAS iliweka vikwazo vikali dhidi ya nchi ya Mali mwezi Januari baada ya serikali ya kijeshi ilipokataa kurejesha haraka utawala wa kiraia. Imetishia vikwazo kama hivyo dhidi ya Guinea na Burkina Faso kama zitashindwa kuwezesha mpito wa haraka kwa utawala wa kiraia ndani ya muda unaofaa.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG